Watu wanaonenenda bila maono, hakika hawana wanalotazamia kutimiza
maishani, na hili limekuwa tofauti - kwani Jumapili tarehe 10 kwenye
parishi ya Mtakatifu James inayoongozwa na Canon Andrew Kajembe, iliyopo
Kaloleni jijini Arusha, dayosisi ya Mlima Kilimanjaro, ambapo kwaya
kongwe nchini, Tumaini 'Shangilieni' ilikuwa ikiweka wakfu DVD yake ya
Nisamehe.
DVD hiyo yenye nyimbo 11 ambayo iliwekwa wakfu na Askofu wa Dayosisi ya
Mlima Kilimanjaro, Stanley Mount Kilimanjaro, iliambatana na changizo
lenye nia ya kukusanya shilingi milioni 65 za Kitanzania, kwa lengo la
kujenga kituo cha kutoa mafunzo ya muziki, ili kundi la vijana, ambalo
ni kundi lenye vipaji mbalimbali vilivyokosa fursa ya kuendelezwa lipate
kujinusuru na changamoto kadha wa kadha za maisha.
Kwa mujibu wa risala ilyosomwa kwa mgeni rasmi, Bi Janeth Jackson Simon
ambaye alichangia kiasi cha shilingi milioni 5, kwaya ya Tumaini ambayo
ina waimbaji 80 na matoleo 11 hadi sasa imeeleza kuwa milioni 65
zitatumika kununua eneo la ujenzi wa kituo hicho ambacho kinatarajiwa si
tu kukuza vipaji kwa vijana, bali pia kupunguza ukosefu wa ajira
nchini.
Zifuatazo ni picha za tukio hilo kama ambavyo GK ilikuwepo na kushuhudia.
|
Barabara ya Kaloleni, lilipo kanisa la St James |
|
Kwaya ya Upendo ikisindikiza kwaya kuu |
|
kwaya ya Mtakatifu Cecilia |
|
Efatha Choir |
|
Askofu wa dayosisi, Stanley Mount Kilimanjaro akihubiri kwenye ibada ya pili |
|
Mama Askofu Stanley, akiwa na mwana, Caleb |
|
Askofu akisindikizwa mara baada ya kumaliza kuhudumu kwenye ibada ya pili |
|
Gari iliyombeba Askofu Stanley Mount Kilimanjaro ikiondoka |
|
Mgeni rasmi, Janeth Jackson Simon akikabidhiwa keki maalumu |
|
Meneja wa mfuko wa jamii wa PPF kanda ya kaskazini akitamka mchango wake |
|
Kwa mzee huyu, maneno yalikuwa machache na vitendo kwa sana. Kwani alishukuru kupata madhabahu ya kuteketezea sadaka yake |
|
Mnada ukaanza |
|
Mchungaji msaidizi akipewa nakala ya DVD mara baada ya kuchangia kwaya |
|
Zawadi kwa mama |
Tumalize kwa kutazåma wimbo mmojawapo uliopo kwenye DVD hiyo, Niongoze Bwana, kama ulivyoimbwa kanisani hapo.
The Complete Guide To Coin Casino | How To Play & Win
ReplyDeleteOnline Casino Games — A basic guide 인카지노 to online casino games. septcasino Read a comprehensive guide to coin 카지노사이트 casino games, including rules, software and how to