Elimu ya Mungu ni NURU isiyokaa ndani
yao watu wabaya; Nao waijuao ndiyo waliofungwa pamoja na Mungu ili
utukufu wake ukae kwao na katika hayo basi;
Tunayo thamani kubwa sana sisi
tulioipata NEEMA ya kuwa hifadhi ya NURU ya MUNGU tujapo kuwa katika
miili hii korofi, miili hii tata, miili hii dhalimu, miili hii yenye
tamaa, miili hii yenye kila aina ya adha yenye kuona kiu, njaa na
kuumwa,
Lakini je sie yaani sisi;
La kutufaa ni lipi? Hakika wema wa Mungu
uliojificha machoni pa wapumbavu ulio wazi kwao wenye uhitaji ndilo
jambo lililo bora saana katika sisi.
Ama ninyi mwaona ni?
Maana kama si katika hilo sisi
tungejivuna katika lipi? Ama umahili wetu wa kulitaja jina la BWANA pasi
na kuyaishi mapenzi yake?
Ni jambo la kumshukuru Mungu wetu ambaye
kwa yeye tumekuwa hivi tulivyo; yaani wenye kunena mema ambayo
twayaishi, wenye kumulika gizani ili kuleta mwanga!
Basi tujitunze mioyo na nafsi zetu
ili tusije tekwa akili na fahamu zetu na ile kawaida ya dunia ikapelekea
sisi kuwa waasi wa ile haki ya Mungu iletayo amani na kujenga furaha
maishani mwetu!
Mbarikiwe.