Habari yako? Siko yako ama ya rafiki
yako inaendaje? Kama basi uko vibaya na unahisi mambo yamekuelemea, ama hata
rafiki yako, si vibaya kuigeukia Biblia, maana ni kitabu ambacho kwetu
sisi Wakristo, kinaonyesha njia. Mistari yake ina uwezo wa kukubadili na
kukufariji pia.
Hivyo basi kama wewe ama rafiki yako
amekuwa na siku mbaya, pitia mistari hii na uitafakari ahadi ya Mungu kwako. John Calahan wa Christian
Post amezikusanya.
1 Petro 5:6-7
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa
Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa
zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
2 Thesalonike 3:16
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na
awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.
Wafilipi 4:6-7
Msijisumbu kwa neno lolote;
bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na
zijulikane na Mungu.
Zaburi 50:15
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa,
na wewe utanitukuza
Mathayo 7:7
Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi
mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa
1 Thesalonike 5:16-18
Furahini siku zote; ombeni bila
kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika
Kristo Yesu.
Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na
amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi
nimeushinda ulimwengu.
Comments/disqusion
No comments