''(Sina maneno ya kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji wake,
pia nawashukuru watu wote walioniombea pamoja na waliokuja kuniona hata
wale ambao wameshindwa kufika, kwani najua walikuwa wakiniombea)''
Hayo ni baadhi ya maneno ya muimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku,
akiieleza GK, kutokana na ajali aliyopata usiku wa kuamkia tarehe 26
Julai 2014. (bofya kuona picha)
GK ilitaka kujua kama kwa sasa anaweza kuinuka na kutembea mwenyewe bila
kusaidiwa na mtu yoyote, ndipo hapo Bukuku akaamua kuionyesha GK kwa
vitendo kwa kuamka mwenyewe na kutembea kisha kurudi tena sehemu
alipokuwa amepumzika.
Bahati Bukuku anasema kwa sasa yupo imara kabisa na yupo tayari kuanza
huduma sehemu mbalimbali ya kumwimbia Mungu. Pia GK imemkuta dereva wa
gari waliyopata nayo ajali, Bwana Edson Mwakabungu akiendelea vizuri, na
kwamba anasubiri baada ya wiki mbili arudi hospitali kutoa bandeji
ngumu au P.O.P. vilevile kijana Frank ambaye aliumia kidogo kichwani ni
mzima na GK haikumkuta bali ilielezwa kwa sasa anaendelea na shughuli
zake kama kawaida
Bahati Bukuku na Silas wa GK. |
No comments:
Post a Comment