Mtumishi Gasper Madumla. |
Imeandikwa;
" Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. " Matendo 3:4
Siku ya leo nataka nikuhubirie kwa kifupi,hasa kwako wewe mtumishi wa Mungu. Yapo mambo mengi ya kujifunza katika utumishi,lakini leo tunaenda kuangalia jambo moja kwa kifupi;
MWAMBATANO WA KIROHO KATIKA KAZI YA BWANA YESU.
Kwanza,nakusalimu;
Bwana Yesu asifiwe...
Nasema,Jina la BWANA YESU lisifiwe...
Sema,Amen.
Tazama katika andiko lilo hilo hapo juu, ( Matendo 3:4 )
Petro angeliweza kumwambia yule kiwete kwamba " nitazame mimi " lakini alijua kwamba haina maana kujiweka peke yake katika huduma ambayo wote walipewa na mmoja Bwana Yesu Kristo.
Mimi sijui hali ingekuwaje kama ingelikuwa leo hii,labda mtumishi angelisema vivyo hivyo kama alivyosema Petro au labda angelisema " nitazame mimi " mimi sijui ingelikuwaje!
Sijui kama unanielewa vizuri hapo!
Ok,labda nikuambie hivi;
Ipo tofauti kubwa kati ya msemo " tutizame sisi " na msemo " nitizame mimi "
Mtu asemapo " nitizame mimi " humaanisha yakwamba mtu huyo yupo peke yake ndio maana husema katika hali ya umoja.
Lakini mtu asemapo " tutizame sisi " wapo wawili tena huwakilisha wingi.
Ndiposa nami nikajifunza jambo moja kwamba ;
Kazi ya Mungu haiwezekani kufanywa na mtu mmoja peke yake pasipo mwingine,maana hata kama mtu atahubiri mwenyewe mwanzo mwisho,basi anamuhitaji mtu wa kusifu na kuabudu,Au hata kama mtu ataabudu na kusifu,pamoja na kuhubiri yeye peke yake basi atahitaji watu wa kusikiliza,watu hao ndio wanakamilisha kazi ile aifanyayo mtu huyo.
Sasa;
Ifike wakati ambapo tutumwapo kazi na Bwana Yesu,basi yatupasa kuifanya kwa umoja wetu katika roho. Kwanza kwa kuonesha tunahitajiana sisi kwa sisi ili kuikamilisha kazi. Maana tu viungo vya Kristo;
Bwana Yesu Kristo mara nyingi alitutaka tuwe wamoja katika kazi yake,tazama anasema;
" Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. " Yoh.17:11
Hata mtunga Zaburi naye anasema;
" Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. " Zab.133:1
Umoja unaozungumziwa hapo ni umoja katika roho,kuitenda kazi ya BWANA MUNGU kwa umoja wetu,tukiwa ndugu wa rohoni. Ndio maana hata Petro aliweza kumwambia yule kiwete " Tutizame sisi "
Lile neno " Tutizame sisi " ( Matendo 3:4) lilikuwa na nguvu ya ajabu maana umoja ule ulikamilishwa na Bwana Yesu mwenyewe, by the way- wakina Petro na Yohana hawakuwa peke yao bali walikuwa na Bwana Yesu pamoja,hivyo kwa lugha nyingine yule kiwete alimtizama akina Petro waliokuwa ndani ya Yesu.
Haleluya...
Haleluya....,Utukufu ni kwa Bwana...
Imeandikwa tena;
" Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; " Marko 6:7
Haleluya...
Ngoja nikuulize swali kwanza,
Hivi unafikiri Bwana Yesu alipowatuma wawili wawili alikuwa hawaamini katika kazi aliyowapa?
Au
Unafikiri kwamba Bwana Yesu alijua kama akimtuma mmoja hataweza kutimiza yale aliyotumwa?
Jibu:
La hasha!
Hata kama angelitumwa mmoja angeliweza kufanya jinsi impasavyo. Lakini aliwatuma wawili wawili kuonesha umoja katika roho ndani ya kazi yake. Siku zote wawili ni wawili tu.
Kupo kusaidiana katika kazi ya Bwana.
Sote tu viungo vya Kristo,hivyo yatupasa kufaidiana kwa kuujenga mwili wa Kristo.
Ukitaka kumuona Bwana kwa viwango vya hali ya juu basi tenda kazi yake pamoja na watenda kazi wote.
• Kwa huduma ya maombi na maombezi ,nipigie;
0655-111149.
No comments:
Post a Comment