skip to main
|
skip to sidebar
GOSPEL IS HOT
Social Icons
Pages
Home
HABARI ZA DINI
SHUHUDA
IJUE BIBILIA
KUWA KIIMANI
NDOA
MAHUSIANO
Popular Posts
HABARI PICHA: KWAYA YA TUMAINI 'SHANGILIENI' YAWEKA WAKFU DVD YA NISAMEHE
Watu wanaonenenda bila maono, hakika hawana wanalotazamia kutimiza maishani, na hili limekuwa tofauti - kwani Jumapili tarehe 10...
KAKA WA KWETU PAZURI,AWEKA HATUA YA UCHUMBA HADHARANI
Nelson na mke mtarajiwa Irakiza Eunice. Kwa wale wadada waliokuwa wakisugua magoti kwa Mungu kupata kibali cha kuolewa na mwanaka...
SHANGWE ZA GK: HARUSI YA MTANZANIA NA MWIMBAJI WA KWETU PAZURI KATIKA PICHA
Jumapili iliyopita huko jijini Kigali nchini Rwanda mwanakaka Warren Bright kutoka Tanzania alikuwa akifunga ndoa ya kimila na mpenzi...
PATA KUJUA ZAIDI: Elimu ya Mungu ni NURU!
! Bwana Yesu asifiwe! Elimu ya Mungu ni NURU isiyokaa ndani yao watu wabaya; Nao waijuao n...
PICHA ZA IBADA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWIMBAJI WA NEW LIFE BAND
Angalia picha mbalimbali za ibada ya mazishi ya aliyekuwa mpigaji ngoma(drums) na mwimbaji wa New life band ya jijini Arusha mareh...
HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASARI YAFANA TAZAMA HAPA PICHA ZAIDI YA 20
Msafara wa gari chache majira ya saa 2:30 ulianza safari katika viwanja vya Usa-River ambako gari za maharusi zilikuwa zikipambwa mdog...
PICHA KAMILI UZINDUZI WA ALBUM YA KAMATA PINDO LA YESU YA ROSE MUHANDO JIJINI DAR ES SALAAM
Angalia picha mablimbali za uzinduzi wa album ya malkia wa muziki wa injili nchini Rose Muhando iitwayo 'Kamata pindo la Yesu...
HABARI PICHA:BAHATI BUKUKU SASA MZIMA WA AFYA NJEMA :ANAMTUKUZA MUNGU
''(Sina maneno ya kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji wake, pia nawashukuru watu wote walioniombea pamoja ...
MISTARI 7 YA BIBLIA KUKUINUA KWENYE SIKU MBAYA
Habari yako? Siko yako ama ya rafiki yako inaendaje? Kama basi uko vibaya na unahisi mambo yamekuelemea, ama hata rafiki yako, si ...
TAARIFA KATIKA PICHA : AFYA YA BAHATI BUKUKU YAZIDI KUIMARIKA NA WALA HAJAVUNJIKA MGONGO
Hali ya mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku inazidi kuimarika na kuendelea vizuri kama GK ilivyomshuhudia akiwa nyumbani kwak...
Sample Text
Followers
Powered by
Blogger
.
About Me
Unknown
View my complete profile
Sample Text
NDOA
No comments:
Post a Comment
Home
Subscribe to:
Posts (Atom)
gospel is HOT
Follow this blog
Blog Archive
Blog Archive
October (1)
September (8)
August (18)
July (28)
June (13)
May (12)
March (13)
October (2)
September (2)
August (19)
TANGAZA NASI
HABARI ZA WIKI HIII
HABARI PICHA: KWAYA YA TUMAINI 'SHANGILIENI' YAWEKA WAKFU DVD YA NISAMEHE
Watu wanaonenenda bila maono, hakika hawana wanalotazamia kutimiza maishani, na hili limekuwa tofauti - kwani Jumapili tarehe 10...
PICHA KAMILI UZINDUZI WA ALBUM YA KAMATA PINDO LA YESU YA ROSE MUHANDO JIJINI DAR ES SALAAM
Angalia picha mablimbali za uzinduzi wa album ya malkia wa muziki wa injili nchini Rose Muhando iitwayo 'Kamata pindo la Yesu...
LEO TUMECHAGUA KUSIFU NA KUABUDU PAMOJA NA MISE ANAEL
Misericordias Anael Mushi Chaguo la GK wiki hii linatoka kwa Misericordia Anael Mushi, ambay kutumia 'saxophone' kumuabudu...
KWA NENO LA MUNGU,NITAZISHUSHA NYAVU
Na mtumishi Gasper Madumla. " Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate...
(no title)
UHUSIANO WA MAGONJWA NA DHAMBI - ASKOFU KAKOBE Askofu mkuu Zachary Kakobe. Leo tena tunaendelea kujifunza Kitabu cha YOHANA katik...
MATUKIO YA JUMAPILI NI UZINDUZI WA DVD YA ARUSHA GOSPEL CHOIR KIJENGE LUTHERAN
Katika matukio yaliyojili makanisani jumapili iliyoisha, tunakuletea tukio moja la uzinduzi wa DVD ya pili ya k...
Moyo wa Mwanadamu!
Mungu anasema mengi sana kuhusiana na moyo. Lakini moyo ni nini? Na umuhimu wa moyo ni nini katika maisha yetu ya kiroho na ya kimw...
MWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURI KABLA HUJAOA
1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama m...
MUIMBA NYIMBO ZA INJILI MAARUFU TZ, HAPPY KAMILI ATUPWA JELA..!
Mwimbaji Maarufu wa Nyimbo za Kumtukuza Mungu, Happy Kamili . Mwimbaji Maarufu wa Nyimbo za Kumtukuza Mungu, Happy Kamili amehukumiwa k...
MO: MASHARTI YA KUMFUATA YESU (MATHAYO 16:21-28) - ASKOFU KAKOBE Askofu mkuu Zachary Kakobe. SOMO: MASHARTI YA KUMFUATA YESU (MATHAYO 16:21-28) Katika MATHAYO 16:21-28, kuna mengi ya kujifunza kwa mwanafunzi wa Biblia. Ingawa kichwa cha somo letu ni “MASHARTI YA KUMFUATA YESU”, ni muhimu kufahamu kwamba hiki ni kipengele kimoja tu katika vipengele vinne vinavyotuongoza katika kuyatafakari yote tunayoyapata katika mistari hii. Vipengele hivi vinne vya somo letu la leo, ni hivi vifuatavyo:- (1) KUTABIRIWA KWA KIFO NA KUFUFUKA KWA YESU (Mst. 21); (2) KUSHAWISHIWA KWENDA MBALI NA MPANGO WA MUNGU (Mst. 22-23); (3) MASHARTI YA KUMFUATA YESU (Mst. 24-26); (4) KUTABIRIWA KWA KUJA KWA YESU MARA YA PILI (Mst. 27-28). (1) KUTABIRIWA KWA KIFO NA KUFUFUKA KWA YESU (Mst. 21) Kifo cha Yesu Kristo hakikuwa kifo cha kawaida. Yesu Kristo hakukutwa na kifo chake bila kufahamu mapema kama wanadamu wengine. Mapema sana, Yesu Kristo, alitabiri na kufundisha jinsi atakavyokufa na kwamba atafufuka siku ya tatu. Alirudia mara kwa mara kueleza hivyo (MATHAYO 17:22; 20:17-19; 26:1-2; MARKO 8:31; 9:31; 10:32-34; LUKA 9:22,44; 18:31-34). Ilikuwa ni mpango wa Mungu, Yesu Kristo kufa. Alikuja duniani ili afe kwa sababu zifuatazo:- 1. Awe ni mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (YOHANA 1:29; 1 WAKORINTHO 5:7; 1 PETRO 1:19; ISAYA 53:7; 1 YOHANA 3:5; WAGALATIA 1:4); 2. Afe kwa niaba yetu, achukue adhabu yetu ya mauti ya milele (WAEBRANIA 2:9; WAGALATIA 3:13; 1 PETRO 3:18). Kufufuka kwake kulionyesha ushindi juu ya mauti. Sisi nasi kwa kumwamini tunapewa kushinda uchungu wa mauti yaani dhambi (1 WAKORINTHO 15:56-57). (2) KUSHAWISHIWA KWENDA MBALI NA MPANGO WA MUNGU (Mst. 22-23) Tunapodhamiria kutekeleza mpango wowote wa Mungu kwetu, ni muhimu kufahamu kwamba watakuwepo watu watakaotumiwa na Shetani kutushawishi kuuacha mpango wa Mungu kwetu. Watu hawa watakuwa watu wa nyumbani kwetu yaani ndugu zetu wa kimwili na kiroho walio karibu nasi. Watatumia maneno ya kutuonea huruma kwa yale yatakayotugharimu au kutupata katika kutekeleza mpango huo. Hatupaswi kuwasikiliza. Siyo wao ila ni shetani anayewatumia. Kazi yetu ni kumtii Mungu na kumpinga Shetani naye atatukimbia (YAKOBO 4:7). MASHARTI YA KUMFUATA YESU (Mst. 24-26) 1. KUJIKANA MWENYEWE KILA SIKU – Kuyaacha mapenzi yetu, furaha zetu na matakwa ya miili yetu yaliyo kinyume na Mungu. Kukataa uhuru wowote ulio mbali na haki na kutafuta kila siku uhuru ulio mbali na dhambi (WARUMI 6:20-22; 8:12-13); 2. KUJITWIKA MSALABA – Tunapaswa kujitwika msalaba kila siku katika kumfuata Yesu (LUKA 9:23). Msalaba ni dalili ya aibu, kudharauliwa, kudhihakiwa, kulaumiwa, kutukanwa na pia kupata maudhi na mateso. Kila siku lazima tukubali kuyabeba haya na kudumu tu katika imani (2 TIMOTHEO 3:12; WAFILIPI 1:29-30; WAKOLOSAI 1:23). 3. KUMFUATA YESU KILA SIKU – Ili tukae na Yesu milele, tunapaswa kumfuata Yesu kila siku, saa na dakika; siyo kwa muda fulani tu wakati wa raha, mahitaji n.k. (YOHANA 10:27). (4) KUTABIRIWA KWA KUJA YESU MARA YA PILI (Mst. 27-28) Kama Yesu alivyotabiri kufa na kufufuka kwake na ikatokea vivyo hivyo, ni muhimu kufahamu pia utabiri huu utatimia wakati wowote ujao. Ni muhimu kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii ili tulipwe kadri ya matendo yetu (1 WAKORINTHO 15:58; UFUNUO 14:13). Katika Mst. 28, wanafunzi wanaotajwa kwamba hawataonja mauti mpaka wamemwona Yesu akija katika Ufalme wake, ni Petro, Yakobo na Yohana ambao walipelekwa juu ya mlima mrefu faraghani na huko wakamwona Yesu katika utukufu wa Ufalme wake (MATHAYO 17:1-2). …………………………………………………………………….. Mpendwa msomaji, unaona sasa! Hakuna haja ya kusema, “Hivi kweli nitaweza kushinda dhambi duniani? Hivi kweli maisha ya wokovu nitayaweza?” Ni Neema juu ya Neema. Unalotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako tu kwa kumaanisha kuziacha; kwa imani tu, na mengine yanayofuata mwachie Yesu; na leo hii utashangaa kuona maisha yako yamebadilika ghafla na kwa urahisi utaona unaweza kufanya mapenzi ya Mungu, bila jitihada za kibinadamu. Je, uko tayari kutubu dhambi zako? Najua uko tayari. Basi sema hivi, “Mungu wangu, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha kuanzia leo. Asante kwa neema yako ambayo kwa hiyo tunaokolewa kutokana na kazi aliyoifanya Yesu. Niokoe sasa na kunipa neema ya kufanya mapenzi yako kuanzia sasa na wakati wote ujao. Asante kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Ili uzidi kuukulia wokovu ulioupokea leo, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!
Askofu mkuu Zachary Kakobe. SOMO: MASHARTI YA KUMFUATA YESU (MATHAYO 16:21-28) Katika MATHAYO 16:21-28, kuna mengi ya kujifunza kwa...
No comments:
Post a Comment