Social Icons

Friday, 1 August 2014

KWA TAARIFA YAKO: HUU NDIO WIMBO ALIOUTUNGA NA KWAYA AMBAYO MAREHEMU KANUMBA ALIKUWA ANAIMBA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu




KWA TAARIFA YAKO mdau wetu wa GK bado tukingali na kwaya ya Neema gospel (N.G.C) ya kanisa la AIC Chang'ombe jijini Dar es salaam, inawezekana unajua au umeshawahi kusoma GK kuhusiana na hili ambalo tunataka kukujuza kwa siku ya leo, kama ufahamu ni kwamba aliyekuwa mwigizaji maarufu nchini marehemu Steven Kanumba kabla ya kuwa mwigizaji alikuwa mwimbaji wa kwaya hii ya Neema gospel ambako licha ya uimbaji pia alishiriki katika shughuli mbalimbali za kwaya hiyo ikiwemo utunzi wa nyimbo pamoja na uigazaji.

KWA TAARIFA YAKO Steven Kanumba alikaribishwa kwenye kwaya hiyo na aliyekuwa mwalimu wa kwaya hiyo bwana Samuel Malonja ambaye kwasasa yupo nchini Marekani, katika mazungumzo yake na GK Samuel alieleza namna ambavyo Kanumba alijiunga na kwaya hiyo "Kanumba akiwa ni muumini wa kawaida, ila mpenzi sana wa kwaya hiyo kiasi kwamba kila baada ya ibada alikuwa akimfuata Sam warudi ndani kanisani ili afundishwe au apige chombo cha muziki. KWA TAARIFA YAKO wakati huo marehemu Kanumba alikuwa na wazo la kupiga gitaa la "bass" na "solo", ndipo akajiunga na kuwa muongozaji wa mdundo (beat) kwa kukaa kwenye "drum" mashine.

KWA TAARIFA YAKO baada ya kufundishwa na kuongeza ujuzi, Kanumba akaanza kuwa mpigaji wa kwaya hiyo, pia akaanza utunzi wa nyimbo, lakini kutokana na upenzi wake wa uigizaji aliamua kujiunga na kundi la Kaole Sanaa Group ambako nyota yake ya uigizaji ilichanua kabla hajajikita kwenye masuala ya uandaaji wa filamu na kusimamia kazi zake mwenyewe. KWA TAARIFA YAKO Kanumba amefanikiwa kutunga wimbo kama ''Ninyi ni nuru'' ambao upo kwenye video ya pili iitwayo ''Pengine hukujua'', lakini pia alishiriki na anaonekana akiimba na wenzake pamoja na upigaji wa vyombo kwenye video ya kwanza ya kwaya hiyo ijulikanayo kama "Dunia imechafuka''.





KWA TAARIFA YAKO Kanumba alifariki dunia huku kukiwa na tetesi za yeye kuandaa album ya nyimbo binafsi ambayo hata hivyo haikuwezekana tena baada ya kifo chake. Ila kwaya aliyokuwa akiimbia bado inazidi kuchanja mbuga katika kumhubiri Kristo kwa njia ya uimbaji, kwani hivi karibuni wameachia album mpya ya sauti iitwayo 'Haki yake Mungu', album ambayo imeleta changamoto mpya katika muziki wa injili kwa ujumla kutokana na kiwango chake, sauti na vyombo kwa ujumla, ili kuelewa nini GK inamaanisha ni vyema ukaitafuta album hiyo kwa kuwasiliana na uongozi wa kwaya hiyo ambayo pia wanapatikana katika mtandao wa Facebook.



Neema Gospel Choir wakiimba katika msiba wa Kanumba viwanja vya Leaders Kinondoni.

Ukitaka kusoma kwa undani zaidi maisha yake wakati akiimba kwaya na wenzake walivyomuelezea

BONYEZA HAPA

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo tukaona bora tukukumbushe kama ulikuwa hujui ama umeshasahau kuhusiana na utumishi wake. Vinginevyo tukutane wiki ijayo..


No comments:

Post a Comment