Mwanamama Nobathembu Mabeka akiwajibika ndani ya Joyous Celebration. |
Wapenzi wa kundi la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini wazidi kupatwa na huzuni na taarifa za waimbaji wa zamani kuendelea kujitoa ndani ya kundi hilo katika siku za hivi karibuni. Wakati huu ambao kundi hilo likingali likiitangaza album yao ya 17 katika ziara waliyoipachika jina la "The Grateful" tayari waimbaji nyota watatu wametangaza kujitoa kundini.
Kati ya waimbaji walioondoka siku za karibuni ni mwanamama mwenye mwili mkubwa Nobathembu Mabeka anayependwa sana na mashabiki wa kundi hilo kwa ustadi wake katika kushambulia jukwaa ambapo ameshindwa kushiriki katika ziara zinazofanywa na kundi hilo ingawa tayari alikwisha maliza mkataba wake siku zilizopita na wakati wote alikuwa akiimba kama mshirikishwa. Wengine waliojitoa ni pamoja na mwanadada Siyasanga Kobese aliyeimba wimbo wa Noyana katika album ya 14 pamoja na wimbo Hay'inyweba album ya 17, Philile Chonko aliyeimba wimbo Solabhelela album ya 15 pamoja na waimbaji wengineo.
Viongozi wa kundi la Joyous Celebration. |
Hata hivyo licha ya malalamiko yote hayo kundi hilo halijaomba radhi kama lilivyotakiwa na mashabiki wake badala yake mashabiki wa kundi hilo kutoka miji mingine wamekuwa wakitaniana na mashabiki wenzao wa Cape Town kwa yaliyowasibu. Kundi hilo kwasasa linaendelea na ziara zao kabla ya kujifungia kumalizia mazoezi ya mwisho tayari kwa kurekodi album ya 18 mwezi December mwaka huu.
No comments:
Post a Comment