Angalia picha mbalimbali za ibada ya mazishi ya aliyekuwa mpigaji
ngoma(drums) na mwimbaji wa New life band ya jijini Arusha marehemu
Eglah Bavuma ambayo yamefanyika jana ijumaa nyumbani kwao mkoani Kigoma
na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo waimbaji wenzake wa New life
band, Upendo Nkone, kwaya ambayo amewahi kuifundisha marehemu wakati
akiwa mkoani Kigoma, wazazi, ndugu jamaa na marafiki.
Baba mzazi wa marehemu mwenye fulana nyeupe akiwa msibani nyumbani kwake mjini Kigoma. |
New life band wakiimba msibani hapo. |
New life band na sura zenye huzuni za kuondokewa na mpendwa wao. |
Mchungaji wa kanisa la Pentekoste Patandi mjini Arusha ambako marehemu alikuwa akiabudu akizungumza machache katika msiba huo. |
Upendo Nkone akiimba kwa uchungu wa kuondokewa na kaka yake. |
Kwaya iliyokuwa ikifundishwa na marehemu kwa takribani miaka 10 kabla hajatoka mkoani Kigoma, ikiimba msibani hapo. |
Askofu Kumenya wa kanisa la FPCT akihubiri katika msiba huo. |
Kiongozi wa New life band Fortunatus Mabondo akizungumza na watu waliofika msibani hapo. |
Baadhi ya umati wa watu waliofika msibani siku ya jana. |
Huzuni ikiwa imetawala. |
New life band walishindwa kujizuia kuonyesha hisia zao juu ya kuondokewa na mwenzao. |
Maua yakiwekwa juu ya kaburi la Eglah. |
Hakika Eglah ameacha huzuni kwa wengi. |
New life band baada ya mazishi wakiwa katika picha ya pamoja©New life band. |
No comments:
Post a Comment