Bahati Bukuku katika mojawapo ya huduma, kwenye tamasha la kwanza mwaka 2014. |
Taarifa za kusikitisha ambazo GK imepata na kuzithibitisha asubuhi hii
ni kuhusu kutokea kwa ajali ya gari iliyomhusisha muimbaji nyota nchini,
Bahati Bukuku maeneo ya Kongwa, Dodoma baina ya gari lake na Lori,
usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane usiku, wakielekea jijini Kahama,
kwenye huduma.
Taarifa za awali zinaeleza kwamba Bahati amelazwa hospitali ya Kongwa
baada ya kuumia mgongo. Dereva wake aliyetambulika kwa jina moja la
Eddy, ameripotiwa kuumia miguu, huku wasindikizaji wawili wa Bahati
awapo jukwaani, wameumia, mmoja kichwani, na mmoja akisalimika kidogo
kiasi cha kubaki eneo la ajali na gari wakati majeruhi wakipelekwa
hospitalini. GK ilipomtafuta Bahati, alipatikana lakini akaongea kwa
shida kwamba hali yao si nzuri kiasi cha kushindwa kuongea vema, na
kuomba mawasiliano yafanyike baadaye.
Kwa hivi sasa ndugu na marafiki wanaelekea Dodoma kwa ajili ya
kufaulisha kuwahamisha majeruhi kwenye hospitali ya Muhimbili. Endelea
kufuatilia Gospel Kitaa nasi tutakufahamisha zaidi, ila cha muhimu
kuliko yote ni kufanya maombi kwa ajili ya mtumishi huyu wa Mungu ili
aendelee kufanya kazi aliyoagizwa hapa duniani - dunia isiyokuwa na
huruma.
Si mara ya kwanza kuripotiwa kwa ajali za magari kutka mkoani Dodoma, kwani mwezi wa tano mwaka huu, muimbaji Edson Mwasabwite alipata ajali akielekea Morogoro kutokea Dodoma, na mnamo mwezi wa nne, mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, naye alipata ajali mkoani humohumo.
No comments:
Post a Comment