Gari waliyokuwemo Bukuku na wenzake. |
Bahati Bukuku akiwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Kongwa. |
Usiku wa kuamkia leo, muimbaji nyota wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku
pamoja na wasaidizi wake, walipata ajali akiwa njiani kuelea Kahama
kwenye huduma. GK ilikuripotia taarifa za awali, na hapa tunakuletea pcha kamili na taarifa rasmi ya jeshi la polisi mkoani Dodoma.
Juhudi za kumhamishia Bahati Bukuku kuelekea Muhimbili kama ilivyopangwa
awali zimeshindikana, kutokana na kushindwa kugeuka wala kuinuka -
akiwa amelazwa. Tayari ndugu na marafiki walishafika kutoka Dar es
Salaam, na watu kadhaa wa Dodoma na viunga vyake walipita kuwajulia hali
na kuwafariji.
Taarifa ya Jeshi la Polisi, Dodoma.
Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU
(31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na
kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine
linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
David Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa
tisa alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya
NARCO Wilaya ya Kongwa.
Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.
Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.
Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.

______________________________________________________________________________________
Frank amesafishwa kichwa na anaendelea vema. Muujiza wake ni kwamba nguo aliyokuwa amevaa ilichanwa na vioo, lakini yeye mwenyewe hajachubuka kutokana na vioo hivyo. |
Jennifer Mgendi (kushoto) akimjulia hali rafiki yake, Bahati. |
Picha zote kwa hisani ya Alpha, ambayealitoka bila kuwa na majeraha
kwenye ajali hiyo, wakati dereva, Eddy (Edson Mwakabungu) yeye
ameripotiwa kuwa mguu umevimba, kiasi cha kulazimika kutoa jeans
aliyokuwa amevaa.
No comments:
Post a Comment