Utangulizi
Leo nimeona niwasilishe makala ambayo ni kutathimini hali halisi ya tabia na mwenendo kila mtu binafsi pamoja na jamii kwa jumla. Na kitu ambacho natamani tukifanyie tathmini kwa kila mmoja wetu ni msamiati wa neno maalum lijulikanalo kama “heshima”! Nataka tulitafakari neno heshima katika maana zake na matumizi yake na kuchunguza ni kwa kiasi gani viwango vyake vinazingatiwa katika jamii ya kizazi hiki.
Na kabla ya kuanza kulitathmini, hebu kwanza tupate tafsiri yake pamoja na matumizi yake asilia. Kwa mujibu wa tafsiri ya Kiswahili sanifu, tunapata maana ya neno “heshima” katika maelezo kama ifuatavyo: 1. Thamani ya utu, utukufu, daraja la juu; 2. Staha, adabu, nidhamu; 3. Kitu anachopewa mtu Kama alama ya kuthaminiwa kwake

Askofu Sylvester Gamanywa |
Msomaji mpenzi, ukifuatilia kwa makini maana ya “heshima” kwa kupitia
maneno yaliyoanishwa hapa juu, unaweza kuigawa “heshima” katika aina kuu
mbili za sifa. Aina ya kwanza ni “sifa za nje” na aina ya pili ni “sifa
za ndani.”
Aina ya kwanza ya heshima ya “sifa za nje” ndiyo inayosababisha wahusika kuonekana kuwa na “thamani ya utu”, au “utukufu” au kuwa katika “daraja la juu”. Mambo haya matatu ndiyo humfanya mtu “kujulikana na wengi katika jamii” (Public figure) au “kuwa maarufu” (famous). Kimsingi “kujulikana” na wengi na kuwa “maarufu” ndiko humfanya mhusika kupata “heshima ya hadhara” (reputation)

Kwa maelezo mengine, “sifa za nje” ni mambo ambayo muhusika amefanikiwa
kuyafanya baada ya kujipatia elimu, ujuzi na kufikia utendaji wa viwango
vya bora vinavyotambulika na mamlaka husika. Kwa kifupi, “sifa za nje”
hutokana na “mafanikio ya nje” na kumfanya mtu kuheshimiwa katika jamii.
Aina ya pili ya heshima ni sehemu ya “sifa za ndani” ambayo hutokana na
“staha”, “adabu” na “nidhamu” Haya mambo matatu yanahusu tabia na
mwenendo wa mtu binafsi kwa jinsi anavyohusiana na watu wengine
wanaomzunguka.
Hizi “sifa za ndani” ndizo zinazo muwezesha muhusika baada ya kupata mafanikio ya “kujulikana” na kuwa “maarufu” kuendelea kujistahi na kustahi wengine, kuwa na adabu na nidhamu binafsi.
Hizi ni “sifa za ndani” ambazo hujenga tabia binafsi ya uadilifu na uaminifu na kuendelea kutunza heshima ambayo ni “thamani ya utu”, “utukufu” na “daraja la juu” katika jamii
Vyanzo vya heshima
Msomaji mpenzi, kama tulivyokwisha kujifunza tafsiri ya msamiati wa neno “heshima”; tumeshuhudia kwamba yako mambo maalum ambayo ni chimbuko na vyanzo vya heshima. Mpaka mtu afikie kiwango cha “kuheshimiwa” mbele ya jamii, lazima awe amefanya mambo na kuonesha ufanisi unaozingatia viwango vya ubora. Baadhi ya mambo ambayo ni vyanzo vya mtu kuheshimiwa katika jamii ni pamoja na:

- Kipaji cha uongozi wenye ushawishi mkubwa katika utawala na utumishi wa umma
- Kipawa cha kiroho katika utumishi wa mambo ya dini
- Elimu ya juu na ujuzi wa kitaaluma
- Hekima na uwezo wa kumiliki mali na utajiri
- Vipaji maalum vya sanaa na michezo
Japokuwa yanaweza kuwepo vyanzo vingine zaidi katika kumfanya mtu
“kuheshimiwa” mbele za jamii, lakini mambo haya matano niliyoyataja
yamebeba uzito wa juu na uchambuzi wangu utalenga haya.
Tunao watu waitwao “waheshimiwa” kutokana na juhudi katika kujipatia elimu na ujuzi wakafanikiwa kupanda madaraja ya kitaaluma na hivyo wakajulikana na kuwa maarufu na hivyo “wakaheshimiwa” na jamii.

Tunao wengine ambao kupitia vipaji vya uongozi walivyojaliwa katika
utumishi wa umma na kwenye madhehebu yetu ya dini, wamejikuta
wamejulikana na kuwa maarufu na wanaitwa “waheshimiwa” kwa misamiati ya
majina ya vyeo na madaraka waliyo nayo katika jamii
Tunalo pia kundi la baadhi ya watu ambao wamejaliwa hekima na uwezo wa
kufanya shughuliza za uzalishaji mali na kumiliki utajiri ambao
umewafanya kujulikana na kuwa maarufu na jamii imewaheshimu kwa sababu
hiyo.
Kana kwamba hii haitoshi, tunalo kundi la wenye vipaji vya sanaa na
michezo ambao wameonyesha uwezo na ubunifu na umahiri katika tasnia za
burdani mbali mbali na kujikuta wamejulikana na kuwa maarufu, na kupata
heshima mbele za jamii inayowazunguka.
Hawa wote, wamejulikana na kuwa maarufu, kupitia vyanzo nilivyovitaja, wakapokea heshima kuliko watu wengine.
Tishio la kujivunjia heshima baada ya kuheshimiwa
Hapo mwanzo tumekwisha kuigawa heshima katika aina kuu mbili za sifa za nje na sifa za ndani. Bila shaka tunaweza kujiuliza ni “Heshima” ipi iliyo bora? Ni sifa za nje au sifa za ndani? Kwa tathmini naweza kusema kwamba “ubora wa heshima” ni muunganiko wa “sifa za nje” na “sifa za ndani”.
Hakuna “ubora wa heshima” unaotegemea sehemu moja pasipo nyingine. Heshima ya umaarufu na kujulikana hudumu tu iwapo wahusika watazingatia tabia za kujistahi, adabu na nidhamu binafsi mbele za watu wanaowazunguka.

Hata hivyo, kwa bahati mbaya, watu wengi wenye kupata heshima zitokanazo
na sifa za nje, baada ya muda si mrefu sana hujikuta wanapoteza heshima
zao mbele ya jamii. Na hata kama wahusika bado wanaendelea kujulikana
na kuwa maarufu kwa kutegemea sifa za nje; lakini wanapoacha kujistahi,
kuwa na adabu na nidhamu binafsi, tayari hupatwa na mmomonyoko wa
maadili ambao huathiri “thamani ya utu” wao, na kuutia dosari umaarufu
wao; na hata kudhalilisha “madaraja ya juu” waliyokwisha kujipatia mbele
za jamii
Heshima ya mtu ili iwe endelevu, lazima ijengwe juu ya "sifa za ndani"
ambazo hutokana na mtu kujizoeza katika mambo ya "staha, adabu na
nidhamu" mambo haya ndiyo humjengea mtu tabia ya uadilifu na uaminifu!
Kwa bahati mbaya "waheshimiwa" wengi hutoa kipaumbele kwa "sifa za nje"
ili kutengeneza umaarufu (reputation); na kisha kupuuza uboreshaji wa
"sifa za ndani" za "staha”, “adabu”, na “nidhamu"; ambazo kimsingi ndizo
huifanya heshima kuwa bora (integrity)
Itaendelea toleo lijalo
No comments:
Post a Comment