Picha mbalimbali zikimuonyesha Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta
pamoja na msaidizi wake William Ruto waliposhiriki ibada jana jumapili
katika kanisa la Redeemed Gospel lililopo Huruma jijini Nairobi ambako
licha ya kushiriki ibada pia viongozi hao walifanyiwa maombi juu ya
ulinzi wa Mungu katika uongozi wao, maombi ambayo yaliongozwa na askofu
Arthur Kitonga wa kanisa hilo kabla ya viongozi hao walielekea katika
kazi zao za chama huko Mathare baada ya kumalizika kwa ibada.
Hii si mara ya kwanza kwa viongozi hao kwenda kuabudu kanisani, kwani wamekuwa na kawaida hii kushiriki pamoja kabla ya kuchaguliwa kwao na hata baada ya kuchaguliwa jambo ambalo limekuwa likipongezwa na wananchi wengi wa taifa hilo kwakuwa viongozi wao wamechagua fungu jema la kumkimbilia na kumtegemea Mungu.

Askofu Kitonga akizungumza na Rais Kenyatta ibadani. |
Mmoja kati ya waimbaji akiimba karibu kabisa na Rais Kenyatta ambaye anaonekana mwenye furaha. |
Rais Uhuru Kenyatta akizungumza na waumini ibadani hapo. |
Baadhi ya viongozi na waumini waliohudhuria ibada hiyo. |
Askofu Kitonga akifanya maombi kwa viongozi hao. |
Maombi yakiendelea juu ya viongozi wa taifa la Kenya.©Rais Uhuru Kenyatta 'Heri Taifa ambalo Bwana ni Mungu wao…. Zaburi 33: 12' |
No comments:
Post a Comment