Kongamano la taifa la 49 la umoja wa wanafunzi wa Kikristo nchini (UKWATA) limeanza hapo jana katika chuo cha ualimu Korogwe mkoani Tanga, likiwa limejumuisha wanafunzi wa sekondari na vyuo vya ufundi nchini na pia unahudhuriwa na maaskofu na wachungaji bila kusahau walimu ambao wamealikwa kufundisha katika kongamano hilo ambalo linatarajiwa kuhitimika siku ya jumapili hii.
Baadhi ya wachungaji na waalimu waliofika katika mkutano huo chini ya Rais wa Ukwata 2013/2014 Joseph Urio ni pamoja na Askofu Dkt Stephen Munga ambaye ndiye alikuwa mgeni mwalikwa, mchungaji Lewis Hizza, mwalimu Grace Masalakulangwa pamoja na mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo na viongozi wengine. Pia katika mkutano huo ambao leo unaingia siku ya tatu tayari Mungu ameanza kutenda kwa wanafunzi hao, ambao hapo jana wengi wao walifunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali vilivyokuwa vikiwakabili.
Katika kongamano hilo wanafunzi watapata nafasi ya kushiriki katika vipaji vya uimbaji, ngonjera, shairi bila kusahau Biblia.
Askofu Dkt. Stephen Munga akijibu risala kutoka kwa wanaukwata katika mkutano huo. |
Waimbaji wakimsifu Mungu katika kongamano hilo. |
Mama Grace Masalakulangwa akifundisha katika mkutano huo wa 49 UKWATA taifa. |
Mchungaji Lewis Hizza akifundisha katika kongamano hilo. |
Rais wa UKWATA bwana Joseph Urio akiwa kwenye tafakuri kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. |
Mchungaji Lewis Hizza akifundisha somo kwa washiriki wa kongamano. |
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akizungumza jambo na washiriki wa kongamano hilo. |
Waimbaji wa shairi kutoka mkoa wa Dar es salaam na Pwani (DARPWANI) wakiwa tayari kwa shairi. |
Majaji wakiandika wakionacho kutoka kwa washiriki wa shindano la kuimba shairi. |
Mashindano ya shairi yakiendelea. |
Baadhi ya umati wa wanafunzi na walimu wanaoshiriki katika kongamano hilo wakifuatilia jambo.©Onai Joseph |
No comments:
Post a Comment