Social Icons

Friday, 13 June 2014

HAPPY KAMILI KUFUNGWA KIFUNGO CHA NJE SOMA HAPA ZAIDI.....


Kifungo cha miezi mitatu jela alichohukumiwa mwimbaji wa muziki wa injili 
nchini Happy Kamili na mahakama ya mwanzo mkoani Mbeya, hatimaye 
kimebadilishwa na sasa kitakuwa kifungo cha nje cha miezi mitatu
 huku akitakiwa kuripoti kwa mkuu wa jela kila siku asubuhi. 
Happy Kamili alihukumiwa kifungo hicho na mahakama ya 
mwanzo mkoani Mbeya kutokana na kuendesha gari 
kizembe wakati anarudi nyuma na kugonga gari nyingine.

Taarifa za kubadilishwa kwa hukumu hiyo ya awali ambayo ilipokelewa 
kwa masikitiko na wadau wa muziki wa injili wanaotumia mitandao
 ya kijamii, imepatikana kupitia kwenye ukurasa wa Facebook ya
 mmiliki wa blogu ya Mbeya yetu bwana Joseph Mwaisango.
 Happy Kamili ambaye ni mke wa mchungaji Athanase
 Kamili wa kanisa la E.A.G.T Isanga Mbeya, amejulikana
zaidi kwenye muziki wa injili nchini kupitia nyimbo zake kama 
'Huwezi kubeba mzigo mwenyewe, Mpango wa Mungu lazima utimie….
 alilopanga Mungu ninani apingee…

Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu blogu ameripoti hivi kupitia 
ukurasa wake wa Facebook


Breaking Newsss mwimbaji wa nyimbo za injiri Happy Kamili 
aachiwa ila ataendelea kutumikia kifungo chake cha miezi 
mitatu akiwa nje ya gereza na kuripoti kila siku asubuhi kwa bwana jela

No comments:

Post a Comment