maombi

Dear wapendwa

Nawasalimu katika jina la Bwana. Mimi ni mkristo ambaye kusema kweli nilikuwa nimepotea kwa maana sikuwa na kweli ya Mungu ndani yangu. Baada ya kupata misukosuko mingi ya maisha nikaamua rasmi kumfuata Yesu.

Nilianza kwenda kanisani mimi na familia yangu  na kwenye maombi pia, tukiwa kwenye maombi msichana wa  kazi akapandisha mapepo na kuanza kusema mambo  mengi ambayo bibi yake, majirani zetu pamoja na ndugu zangu huwa wanaifanyia familia yangu ni vitu vingi sana. Baada ya maombi mchungaji akanisihi sana nisianze kugombana na watu waliotajwa  kuwa wanaifanyia mabaya familia yangu kitu ambacho hata mimi najua siruhusiwi kufanya kwa kuwa hata mimi ni mwenye dhambi mbele za Mungu.

Sasa swali langu wapendwa nataka kujua je mtu anapokuwa amepandisha haya mapepo wakati wa kuombewa yale mambo anayoyasema ni  ya kweli? kuna mda nilikuwa nasikia mpaka tone ya sauti za ndugu zangu kama ndio wanaongea wenyewe, imenichanganya sana sio kwa sababu nataka kulipiza hapana nataka kujua ukweli ili hata kama nawaombea niwe najua wamefanya kweli.