Social Icons

Wednesday, 9 July 2014

MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUONGEZA THAMANI KWENYE MAAMUZI YAKO YA KILA SIKU MAISHA YAKO BINAFSI


1. Punguza Muda wa Kuhudhuria Matukio Mbalimbali
Kizazi chetu ni Event Oriented yaani usipokuwa mwana matukio unaonekana wa namna yako.Hakikisha unajenga tabia ya kupunguza Muda wa kuhudhuria matukio mbali mbali si lazima kila tukio uhudhurie.Hakikisha unakuwa personal reflection time kuhusu mambo yanayokuzunguka maishani mwako.Je utahudhuria matukio mangapi,Matukio pia hayaishi uliyakuta na utayacha lakini maisha yetu yana ukomo na yamejengwa katika vipindi maalumu.Ni muhimu kujenga utaratibu wa kureflect mambo yako Binafsi.Haimaanishi uwe mchoyo bali tumia ufahamu na uelewe wa namna ya kuchagua uhudhuriaji wa matukio. Je kila tukio unalohudhuria lina faida kwako?Je kila tukio lina value gani kwenye maisha yako binafsi? Unaweza ukawa na idadi kubwa ya matukio kila siku lakini yasiwe yanaongeza thamani ya maisha yako wewe binafsi. Tambua ulikuja pekee yako na utaondoka pekee yako hakuna atakayebeba mzigo wako.
2. Punguza Lundo la Marafiki/Makundi
Huwezi kuwa na urafiki ya kila mtu na huwezi kuwa na ukaribu na kila mtu.Unaweza ukaongea na kila mtu na kuishi na kila mtu lakini haikujengei mtu huyo kuwa rafiki yako.URAFIKI ni Zaidi ya Salamu na Kujua umeamkaje na kulalaje. Iwapo mtu hana Personal Intimacy Relationship huyo sio rafiki ni mtu kama watu wengine tu. Tofauti huyu unaongea naye na hao wengine haujapata fursa ya kuongea nao. Chagua watu wachache wanaokufahamu vizuri Huku ukianza na watu wa familia yako then wengine wafwate ndio uwashirikishe maisha yako na maamuzi yako. Usipende kila mtu ajue jinsi ulivyo kila wakati.
3. Tafuta Muda wa Kuongea na Watu Waliokuzidi Umri
Jaribu kutafuta watu ambao wamekuzidi umri karibia mara mbili yako kwa Maana Nyingine Inaweza kuwa Babu/Bibi yako au mtu mwingine mwenye Busara. Muulize hadithi za maisha haswa aliposhinda na aliposhindwa na kwanini? Nyakati.zinaweza badilika na teknolojia inakua lakini Kanuni za Msingi za maisha huwa hazibadiki. BUSARA NA HEKIMA HUDUMU KWA MUDA MREFU LAKINI FEDHA NA MALI HUJA NA KUONDOKA.Usitumie Muda mwingi kufikiria pesa while kuna Zana nyingine muhimu kwenye maisha ambazo zinaweza kukuvusha.
Unaweza ukawa umesoma sana na unajua mengi lakini tambua life will handing us over the same fate.Epuka ujuaji mwingi,hekima husikiliza na elimu hupiga makelele.
4. Jenga Tabia ya Kupenda, Kusamehe na Kuwaamini Wengine
Tunaweza tusiwe tunaongea lugha moja wala kufanya kitu aina moja kwa wakati mmoja lakini Upendo ndio kitu kinachuunganisha kwa Pamoja.Unaweza ukakataa kumsaidia mtu leo lakini kesho ukamhitajia unaweza ukamuona mtu hana thamani kwako leo lakini kunawakati kile alichonacho kinaweza kukusaidia
Hakikisha unajenga tabia ya kusamehe na kuwaamini wengine.Epuka kujenga hoja kwenye matukio ya kusikika.Unaposikia jambo mtatufe muhusika halisi msikilize kile atakachokwambia kiamini haijalishi mazingira yanaruhusu au la .Iwapo.si ukweli kwa wakati wake utagundua usilazimishe kusikia kile unachokipenda wewe. Hii itakujengea kupunguza chuki kwa wengine na kuwasikiza bila jeuri wala kiburi.
5. Dhibiti Mihemko na Hisia Zako Kadri Siku Zinavyoongezeka
Ili uwe mtendaji mzuri na mwenye maamuzi bora imekupasa kujifunza kuzibiti mihemko. Njia nzuri ya kudhibiti mihemko kama mkristo ni maombi na mifungo ya muda mrefu iliyojengwa kwenye msingi wa neno la Mungu. Hii itakupa muda mzuri wa kumsikiliza Roho Mtakatifu nini anakuelekeza cha kufanya na sababu utakuwa tayari na uwezo wa kudhibiti mihemko na maamuzi ya hisia utatekeleza kile anachokwambia na kitakuwa na faida kwako.
6. Punguza Shughuli (Activities) na Ubusy
Mara nyingi tumekuwa na shughuli nyingi ingawa si vibaya ambazo huenda nyingine hazina ulazima. Mara nyingi watu ambao hawana muda binafsi wa utulivu huwaga wana hasira za hapa na pale lakini wanakuwa na Maamuzi ya Muda ambayo huwa hayatatui tatizo la kudumu.Ondoa shighuli ambazo hazina ulazima na ikiwezekana nyingine zikatae,wewe ni mtu mmoja huwezi kufanya kila kitu waachie wengine.Iwapo unaona una vyeo vyingi punguza wachie wengine maana mwisho wa siku unaweza kuwa kituko achia wengine wafanye kwa ufanisi zaidi ili uweze kujenga muda binafsi wa kuwa na reflection ya maisha yako.
7. Epuka Kufanya Maamuzi Yatokanayo na Mitandao ya Kijamii (Facebook, Twitter, Google, Whatsapp etc) Pamoja na Social Media (T.V, Radio etc)
Kizazi chetu tumekuwa na tunashindwa kufanya maamuzi mengi yalio mazuri sababu hatuna Muda binafsi wa utulivu sababu utakuta muda mwingi tunaiamini mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuliko tunavyojiamini wenyewe bila kujua Vyombo vya Habari na Mitandao hio iko kimaslahi zaidi iwe moja kwa moja au isiwe ..Hata iwapo wewe binafsi utaharibikiwa au kufanikiwa wao haiwahusu sana so ni muda muafaka wa kuhakikisha unakuwa na muda wa kuchuja na kuangalia yale yaliopo kwako binafsi bila kuangalia ushawishi kutoka kwenye Mitandao ya Kijamii au Vyombo vya habari ingawa ni muhimu kusikiliza lakini visiwe ndio muamuzi wako wa mwisho.Pia Epuka kupelekea matatizo yako mengi na changamoto zako kwenye Social Media na social Networks ili kupata public sympathy na suluhisho la kile unachopitia.Hii itakusaidia kuepuka pressure kwenye maamuzi yako mengi.
Tukutane wiki ijayo,

No comments:

Post a Comment