Kauli hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nje na
mahusiano wa Cameroon mheshimiwa Henri Eyebe Ayissi katika waraka wake alioutoa
mapema wiki iliyopita ukiwa na kichwa cha habari kisemacho 'shetani yupo ndani
ya nyumba' akimaanisha mtume TB Joshua kwa kumuita mtoto wa shetani akijofanya
ni mtumishi wa Mungu.
Waziri huyo amewaonya mamia ya wananchi wa Cameroon
wanaokwenda kusini magharibi mwa jiji
la Lagos nchini Nigeria kwaajili ya miujiza
kanisani kwa TB Joshua kuachana na safari hizo kwani matokeo yeyote
watakayopata itakuwa juu yao wala nchi yao haitasimama kuwatetea. Waraka huo
ambao umeandikwa kwa lugha ya kifaransa (Cameroon wanazungumza kifaransa) hapa
ukiwa umetafsiriwa kwa kiingereza “The Ministry of Foreign Affairs warns
those who by naivety or deception of Emmanuel TV’s captivating images, or even
those who by hopelessness, envisage taking the pilgrimage to Pastor TB Joshua’s
Synagogue Church Of All Nations in Lagos, that they will do so at their own
risk". ameandika waziri hugo.
Aidha ameongeza kwamba hali ya wanaume na wanawake
wa nchi hiyo kwenda kwa mtume Joshua ni tabia yao ya kupenda miujiza na
wanapokuwa ndani ya kanisa hilo wanajikuta katika hali ya kudanganywa na kubaki
kama wanyama. "wanawake wanabakwa na kunyang'anywa vitu vyao na
wanyang'anyi na kuachwa wakilala mitaani bila msaada, matukio mengi ya mauaji
yamerekodiwa na haya ni mbali na matukio ambayo hayajarekodiwa katika ubalozi
wa Cameroon jijini Lagos kwasabau wahusika wanaona aibu kuyaeleza
yaliyowakumba" amesema waziri huyo.
Waziri huyo akaenda mbele zaidi kwakusema wakati
Biblia inasema kuwasaidia maskini, TB Joshua anaonekana kila leo akigawa mabegi
ya mchele kwa watu wenye uhitaji. Wakati huohuo gazeti la Cameroon katika
ripoti yake wiki iliyopita limeandika mamia ya wananchi wa nchi hiyo wamekuwa
wakiuza mali zao zikiwemo nyumba, mashamba au kukopa pesa wakitarajia kupata
miujiza kutoka kanisani kwa TB Joshua lakini wanaishia kukata tamaa wanapofika
Lagos.
Magazeti yameandika kwamba runinga ya mtume huyo
imekuwa maarufu sana nchini Cameroon kwakutazamwa na waengi na kufanya wengi
kupata majaribu ya kusafiri kwenda kwa mtume huyo ili kupata uponyaji ama
baraka. Gazeti hilo limeandika kwamba kwasasa mtume huyo anatazamwa takribani
kila nyumba nchini humo na kuamini miujiza yote wanayoiona kupitia runinga huku
gazeti moja likimnukuu mmoja wa watu waliokwenda kwa mtume huyo na kurejea
kwamba ameweza kuokoa ahadi yake na mtumishi huyo wa Kristo na kwamba pesa
aliyotumia kiasi cha shilingi 150,000 za Cameroon (FCA) imekuwa ikiongezeka
kutegemea na matibabu na hali ya mgonjwa, hali iliyosababisha kutoelewana kwa
wananchi wa nchi hiyo na kufunga safari hadi kanisani kwa mtume huyo lakini
matokeo yake wanageuka wakimbizi kwenye ubalozi wao uliopo Lagos.
Hii si mara ya kwanza kwa Cameroon kutoa tamko la
kuwakataza wananchi wake kwenda nchini Nigeria kwa mtume huyo ambaye amekuwa
akipata upinzani katika baadhi ya nchi barani Afrika ikiwemo Zimbabwe ambako
kuna taarifa inasema nchi hiyo haitaruhusu mtume huyo kukanyaga ardhi yao
ingawa kuna fununu kwamba mtume huyo anapanga kwenda katika nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment