Social Icons

Friday, 8 August 2014

KWA TAARIFA YAKO: HUYU NDIYE MUIMBAJI ALIYEZALIWA KABLA YA MUDA NA KUTAKIWA KUTUPWA

Haya msomaji wetu wa Gospel is Hot karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.

Miriam Thomas Chirwa mwenye umri wa miaka 16 kwa sasa, ni mtoto mwenye kupenda sana kwenda kanisani kiasi kwamba anaweza kulia hata akiwa shule, hadi atakapokuja kuchukuliwa na baba yake. (kwa kuwa anasoma boarding, na kurudi nyumbani kila Ijumaa.)

Mtoto Miriam Chirwa katika mojawapo ya huduma kwa watoto wenzake. ©Othman Michuzi
Pamoja na umbo lake dogo, Miriam alikuwa na kipaji cha uimbaji tokea akiwa mdogo, kwani KWA TAARIFA YAKO, akiwa na umri wa miaka miwili na nusu tu, na kutokea hapo kuendelea na uimbaji huo kanisani hadi baba yake alipomtungia nyimbo akiwa na umri wa miaka 6. Na hapo ndo mwanzo wa kurekodi albamu yake ya kwanza.
Katika huduma yake ya uimbaji, Miriam alikuwa pia akienda kuimba kwenye shule mbalimbali, hadi pale siku moja mwalimu mkuu wa shule mojawapo aliuliza, "huyu mtoto anasoma darasa la ngapi?" Baada ya kutambua kwamba hajaanza shule, KWA TAARIFA YAKO ndipo hapo shule ikaanza, darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 8.
Pamoja na umbo lake dogo, Miriam shauku ya Miriam ni kubaki hivyo hivyo, na si kuwa kama watu wengine. Na KWA TAARIFA YAKO, Miriam anataka kuwa mwanasheria wa kutetea haki za walio na ulemavu, kwani kwa kufuatilia vyombo vya habari amegundua kwamba wengi wananyanyaswa na hata kutupwa na kuuliwa kutokana tu na namna walivyo.
Miriam hayuko peke yake nyumbani, kwani ana mdogo wake aitwaye Obadiah, ambao KWA TAARIFA YAKO hucheza pamoja hucheza mpira wa miguu, na hata kusimuliana hadithi mbalimbali. Matatizo ya macho ya Miriam, hayajazuia upendo kwa kaka yake, ambaye pia ana ulemavu.


Baadhi wa 'wazazi' hutupa watoto mara baada ya kujifungua, kutokana na visingizio mbalimbali ikiwemo kutojiandaa ama kwamba mtoto ana ulemavu. KWA TAARIFA YAKO kumekuwa na watu wengi ambao walikuwa wanamshauri Baba Miriam amtupe huyo mtoto kutokana na kuzaliwa kabla ya muda (njiti) na pia akiwa na matatizo ya macho, lakini kalenda ya Mungu si kama ya mwanadamu, na kilichopata kibali mbele za BWANA Yesu, hakuna wa kupinga.


Kama ambavyo Miriam amefanyika baraka kwa jamii, licha ya muonekano wake, wewe unafanya nini juu ya maisha ya wengine? Unawawazia nini wenzako? Unajilimbikizia kiasi gani? Umesaidia jamii yenye uhitaji? Unamtumikia BWANA kwa namna gani? Unaisogeza injili kwa mfumo upi? Basi pamoja na hayo, KWA TAARIFA YAKO tambua ya kwamba unaishi kwa Wema wake Yesu, na sio kwa akili zako.
Hiyo ndiyo KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment