Social Icons

Thursday, 15 August 2013

ALBUM MPYA YA BAHATI B-SIJAMSHIRIKISHA MTU KWAKUWA SIJUI KIUJAZACHO MOYO WAKE KUTAMKA YESU SIO KAZI


Namshukuru Mungu niko kwenye hatua za mwisho kabisa kumalizia album yangu ambayo itakuwa na nyimbo kumi au nane kutokana na nafasi,yaani ni nyimbo kama tatu hivi namalizia kwasasa kwenye tarehe 25 mwezi huu natarajia kuzisambaza kwenye vituo vya radio ili zianze kusikika'' hilo ndilo jibu la mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Bahati Bukuku wakati akijibu baadhi ya maswali wakati akizungumza na HABARI na BURUDANI.

      Bahati Bukuku akimtukuza Mungu katika moja ya mialiko ya harusi aliyoalikwa .

 Ikiwa takribani miaka mitatu tangu mwimbaji huyo kutoa album yake ya tatu iitwayo ''Nimesamehewa dhambi sio majaribu'' iliyojaa nyimbo nyingi zenye ujumbe mzito kama wimbo uitwao Waraka wa Hamani ambao mpaka sasa bado wapenzi wa muziki wa injili wameendelea kuupigia chapuo kwamba hakika ujumbe umesimama.

                       Bahati Bukuku katika hali yake ya kawaida



 Habari na Burudani  ilipomuuliza ni kwanini amechukua muda mrefu kutoa toleo jipya kama ilivyokuwa waimbaji wenzake wa injili,Bahati amesema ni suala la wakati hawezi kufanya mambo kwa kuiga wengine wanafanyaje kwakuwa hajui mkataba na boss wao(Mungu) ukoje yawezekana wanatakiwa kutoa kanda kila mwaka,ila kwake yeye ni tofauti kwa jinsi roho wa Mungu anavyomuongoza,'' pia katika hali ya ubinadamu unatakiwa usome alama za nyakati uangalie ni kitu gani kinaendelea katika maisha ili upate kuomba Mungu akupe mwongozo wa kitu cha kuponya roho za watu,huu si wakati wa kukurupuka tu kuchukua maneno ya mitaaani unapachika kwenye nyimbo za injili, maneno matatu tu yanajirudia kwenye wimbo watu wanacheza dansi hapo hata ujumbe wa kuponya roho zao hamna maana hata mwimbaji mwenyewe ukiangalia video yake amesakata dansi kwahiyo utakuta muziki wa dunia na gospel hakuna tofauti kitu ambacho ni hatari.

 Habari na burudani ilipomuuliza kama kamshirikisha mwimbaji mwingine katika album yake,Bahati amesema hajamshirikisha mwimbaji yeyote na wala hafikirii kwakuwa hata Mungu hajamuongoza kuhusu hilo kwasasa labda hapo baadae kwakuwa hajui huyo anayemshirikisha amebeba nini rohoni mwake na nini hasa dhima yake katika uimbaji wa nyimbo za injili, maana muda mwingine Mungu anashindwa kuongea nawewe kutokana na huyo unayeandamana naye akitolea mfano kwa Ibrahimu na  Ruthu walipokuwa pamoja Mungu alishindwa kuzungumza direct na Ibrahimu mpaka pale kila mmoja aliposhika njia yake ndipo Mungu alipoanza kuzungumza na Ibrahimu,ingawa Mungu ameagiza umoja ni kweli kabisa nina umoja na upendo na waimbaji wenzangu wa injili lakini katika suala la kumshirikisha mtu kwenye album yangu bado hata album ikiwa mbaya nitajijua mimi na Mungu wangu, na kwa mtu anayetaka kunishirikisha kwenye album yake niko tayari hasa kwa wale ambao roho wa Mungu ananishuhudia kushirikiana nao,ninakwenda kushiriki katika album yake kwakuwa ndani yangu najua ninani ninayemtumikia,maana siku hizi kumtaja Yesu kwenye uimbaji sio issue kila mmoja anayomaana ndani yake.
aidha Habari na Burudani ilipotaka kujua kama kuna mtu anamsaidia kutunga nyimbo zake, Bahati amesema hakuna mtu zaidi ya yeye mwenyewe na Mungu wake kwamaana amesema hawezi kuimba kitu ambacho hajakipitia wala kuwa na uhakika nacho kwa maana nyimbo zake zote anazoziimba ni maisha halisi aliyopitia,anayoyaona kila siku kwahiyo hawezi kuimba wimbo wa kutungiwa na mtu kwakuwa hata kuimba kwake kutakuwa kimaigizo zaidi kama ilivyo mtu anayeimba jukwaani kwakutumia cd,kwahiyo ndugu yangu Habrai na Burudani situngiwi wimbo na mtu ni mimi na Mungu wangu.
pia Bahati amesema wimbo alioutoa mwaka jana uitwao Lazima usamehe hautakuwamo kwenye album mpya.

 Aidha licha ya album mpya anayotarajia kuitoa hivi karibuni,Bahati anatarajia kutoa surprise ambayo haijawahi kutolewa na mwimbaji yoyote wa injili nchini, kwahiyo amewataka wapenzi wa muziki wa injili nchini na nje ya nchi kukaa tayari kupokea kutoka kwa Mungu pia kuhusu kilichoujaza moyo wake ambacho amesema yeye kama binadamu wengine anayohaki ya watu kumuelewa na kuheshimu mawazo yake,Bahati Bukuku alianza kujulikana kwenye muziki wa injili mara baada ya kutoa album yake ya kwanza iliyofanya vyema sana iitwayo Ni nyakati za mwisho iliyobeba ujumbe mzito kuhusiana na ajali ya treni huko mkoani Dodoma,wimbo kama Mapito na nyingine nyingi, album ya pili inaitwa Nani aitikise dunia iliyo na wimbo ambao pia ulifanya vyema sana alipoingia jerusalem walimwita mbarikiwa alipofika goligotha wakasema asurubiwe na album yake yatatu ambayo bado inafanya vyema inaitwa  Nimesamehea dhambi sio majaribu yenye nyimbo kadha wa kadha kama Majaribu,heshima ya dhahabu,waraka na nyingine nyingi. kaa tayari kusikia ujumbe wa neno la Mungu kutoka kwa Bahati Bukuku.
, 0225509587. Powered by Blogger.

No comments:

Post a Comment