Social Icons

Sunday, 18 August 2013

MASANJA AMPONGEZA MATUMAINI KUOKOKA AMTAKA KUFUMUA BREKI ZOTE ILI ASONGE MBELE


Masanja kushoto akiwa na pacha wake Silas Mbise.
Wiki moja tangu mchekeshaji maarufu nchini aitwaye Matumaini kutoa wimbo wake wa kwanza wa injili wa kumshukuru Mungu kwa kumponya na ugonjwa mbaya ambao ulimpata akiwa nchini Msumbiji, mchekeshaji mwenzake Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji amempongeza mwigizaji mwenzake huyo kusonga mbele na kutokatishwa tamaa na watu wengine juu ya uamuzi wake wa kumpa Kristo maisha yake.

Masanja amesema anajua Matumaini ametendewa jambo kubwa na Mungu la uponyaji wa afya yake na kumtaka kuendelea kung'ang'ania wokovu huo kwakuwa uamuzi wake si kutaka kufurahisha watu bali Mungu na kwamba watu wengi wataanza kumsema vibaya juu ya uamuzi huo, na kwambia kama ameamua kuokoka anatakiwa kufumua breki zote ambazo zitamzuia katika maisha yake ya wokovu. Masanja ameendelea kusema kwamba kumekuwa na wasanii wengi waliotangaza kuokoka lakini wakarudi nyuma, lakini ni maombi yake kuona Matumaini anasonga mbele na asubiri kuona baraka za Mungu juu ya maisha yake "jiandae kuolewa hata kama watu watasema hana umbo namba nane ataolewa tu na hao wenye namba nane watabaki wakishangaa, watu wakisema hutaolewa kwasababu ni mweusi wala usiwasikilize kwakuwa utaolewa na watabaki na weupe wao bila kuolewa.

Matumaini akiwa kazini. Picha kwahisani ya Freebongo.blogspot.com



Aidha Masanja ambaye alikuwa akiyaongea yote hayo kupitia kipindi cha Gospel Celebration ndani ya WAPO Radio Fm kama alivyohojiwa na pacha wake Silas Mbise wakiwa jijini Mbeya kwenye tamasha la muziki wa injili amewataka vijana, wasanii wengine na watu wote kwa ujumla kufanya uamuzi wa kumpokea Kristo sasa sio mpaka waugue au wapatwe na shida ndipo wafanye uamuzi huo kwakuwa ufalme wa Mungu utatekwa na wenye nguvu. Matumaini ametoa wimbo wake alioupa jina la "Nimepona" aliomshirikisha mchekeshaji mwenzake aitwaye Kiwewe, Mkono wa mkonole pamoja na mwanamama Jane Miso aliyeimba vyema kiitikio katika wimbo huo.

No comments:

Post a Comment