Social Icons

Saturday, 17 August 2013

MUNGU NI MWEMA ALIYEKUWA MCHEZA FILAMU ZA NGONO MAARUFU AELEZA ALIVYOKUTANA NA MUNGU

Brittni Ruiz akiwa na tabasamu akieleza Misri ilivyomtesa huku akitumia jina bandia la Jenna Presley. Picha kwahisani ya YouTube.
Binti wa miaka 26 aitwaye Brittni Ruiz ambaye alikuwa nyota na maarufu katika tasnia ya uchezaji mikanda ya ngono akifahamika kwa jina bandia la Jenna Presley ameweka hadharani ushuhuda wake wa jinsi shetani alivyomtumikisha kwa takribani miaka saba akifanya na kurekodi mikanda zaidi ya 275 ya ngono na wanaume tofauti.

Brittni ameamua kutoa hadharani ushuhuda huo ikiwa pamoja na kutaja jina lake halisi akihojiwa na mwanadada Rachel Collins wa XXX Church ikiwa ni mwaka mmoja tangu ampokee Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. Amesema kutokana na muonekano wake pamoja na mafanikio hayo katika utumwa huo wa shetani alikuwa akirekodi zaidi ya mara tatu kwa siku mikanda ya ngono hali iliyomfanya pia kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe kali ili kuendana na maisha hayo ambayo yalimfanya mara nyingi atake kujiua.


Ambapo katika video hii Brittni ameelezea jinsi alivyojiingiza katika maisha hayo akiwa na miaka 18 na mambo yalivyokuwa mpaka Kristo alivyobadilisha maisha yake. akihojiwa na Rachel Collins ambaye walikutana naye kwenye danguro alikokuwa akijihusisha na mambo hayo.

No comments:

Post a Comment