Pata shuhuda za matukio yaliyotukia katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe jijini Dar es salaam pamoja na mkoani Morogoro. Kama GK ilivyoyapata kupitia kurasa ya Facebook ya kanisa hilo.
MCHAWI AUMBUKA KANISANI UFUFUO NA UZIMA
Ni kawaida ya wachawi kujihudhurisha na kujaribu kupima nguvu ya watumishi wa Mungu; ni kweli kuwa baadhi yao huja kanisani kutafuta msaada wa kiroho juu ya kujinasua na roho za uchawi lakini wengine kwa makusudi huja ili kuwafuatilia wale waliowafunga wasifunguliwe.
hiki ndicho kilichotokea wakati Mchungaji Gwajima anamuombea msichana, mmoja na kugundua kuwa mwanamke aliyekaa pembeni yake alikuwa anashindana naye ili yule binti asifunguke. Kwa kujawa na ROHO Mtakatifu Mch. Gwajima alimtambua na kumdhihirisha kwa watu wote.
Najua baadhi mtashangaa ni nini hiki lakini katika biblia Paulo alikuwa akimuhubiria mtu mmoja lakini kumbe pembeni yake kulikuwa na mchawi anashindana na Paulo, kumwingizia roho ya kuacha. "Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. " Paulo akampiga upofu.
Jambo hilo ndilo lililotokea jumapili hii wakati Mch. Gwajima anazunguka katikati ya makutano akiombea watu.
PICHANI NI PICHA YA HUYO DADA NA MCHAWI ALIYEUMBUKA, NA BAADAYE KUOMBEWA NA RP ADRIANO KUFUNGULIWA
Na Mwandishi wetu |Morogoro |Alhamisi |01/08/2013
Mchawi mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alikutwa akiwa amedondoka eneo la nanenane mjini morogoro.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea usiku wa kuamkia alhamisi mara baada ya Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima tawi la Morogoro mjini Dr Godson Issa Zacharia kuongoza majeshi siku ya jumatano kwenye ibada kuliteka anga la morogoro na kuweka msimamo kuwa mchawi yeyote atakayeruka kwenye anga la morogoro usiku huo anaswe.
Katika tukio hilo kijana huyo ambaye umri wake unakadiriwa miaka 17 na 18, baada ya kudondoka hali akiwa uchi wa kuzaliwa, alichukuliwa na askari polisi na kumpeleka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro. Mara baada ya kufika hospitalini hapo, taarifa zilimfikia Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Ufufuo na uzima Dr Godson ambaye akawasiliana na mtendakazi wake ngazi ya Shepherd Dr Gershom amabaye alienda kufanya mahojiano na huyo mchawi.
Alisema kuwa yeye ni mwenyeji wa Shinyanga, usiku huo alitoka pamoja na babu mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake pia kulikuwa na wachawi wengine wengi walitoka pamoja kwenda mpaka mkoani mbeya, na walipotoka mbeya wakaenda hadi baharini na walipotoka baharini iliwabidi waje mkoani morogoro kuhudhuria kikao. Anadai kuwa walipofika eneo la morogoro walikumbana na shida (ambayo hakutaka kuitaja) alidai kuwa ililazimu yeye adondoke ili awanusuru wengine lasivyo kungekuwa na madhara makubwa kwenye kundi zima, hivyo kiongozi wa msafara huo alimshurutisha awe kafara ili wenzake wapone.
Aidha alipoulizwa daktari wa wodi hiyo kuwa mwanga huyo wao wanamhudumia kama mgonjwa mwenye shida Gani? Daktari huyo (jina lake tumelihifadhi) alisema wanamtibu kama mgonjwa mwenye tatizo la akili la muda mfupi (Acute Psychotic Disorder).
UFUFUO NA UZIMA-MOROGORO
No comments:
Post a Comment