Sehemu ya watu waliofika jioni kwenye msiba, EAGT Temeke. |
Hatimaye ratiba kuhusu maazishi ya aliyekuwa askofu mkuu wa makanisa ya
Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Moses Kulola, imetoka na
inaonyesha kuwa maazishi yatafanyika Mwanza siku ya Jumatano Septemba 4
kwenye kanisa la EAGT Bugando.
Akitoa taarifa hiyo eneo ambapo msiba umewekwa, EAGT Temeke, katibu wa
EAGT kanda ya Mashariki Kusini, Askofu Alphonse Mwanjala ameeleza kuwa
kutakuwa na ibada za maombolezo hadi Ijumaa na kwa siku ya Jumamosi
mwili utawasili Temeke kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa mchana
ambapo utaagwa na hatimaye kupelekwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Nyerere kwa ajili ya kuusafirisha siku ya Jumapili kuelekea Mwanza.
Na huko Mwanza pia taratibu nyingine zitafanyika na hatimaye mwili kupumzishwa siku ya Jumatano EAGT Bugando.
Christ Gospel Messengers watakuwepo Temeke na kufanya mkesha kwa siku zote hadi mwili utakaposafirishwa.
Askofu David Mwasota, katibu mkuu wa baraza la makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT). |
Katika mahojiano na Gospel Kitaa, Askofu Mwasota ambaye pia ni mtoto wa kiroho wa Askofu Kulola,
amesema kuwa ni vema viongozi wa makanisa
wakajitokeza ili kufanikisha zoezi la Mzee Kulola ambaye ametumiwa na
Mungu kwa namna ua kipekee katika kueneza injili kwa mataifa yote.
Gospel Kitaa itaendelea kukujuza kinachoendelea hatua kwa hatua.
No comments:
Post a Comment