|
Mtume Onesmo Ndegi, mwenyeji wa Kongamano hilo |
Zilikuwa ni siku sita za kwenda viwango vya juu katika Jiji la Dar es
salam Katika Kanisa la Living Waters Centre chini ya mtumishi wa Mungu
Mtume Onesmo Ndegi, kwenye 'Kongamano la Viwango vya Juu' (Higher Levels
Conference)
Kila mwaka kwenye Kanisa la Living Waters Centre huwa kuna Kongamano kuu
ambalo linakuwa na watumishi wa Mungu kutoka makanisa mbalimbali nchini
na nje ya nchi, ambapo kwa mwaka huu alikuwepo Askofu Kameta wa Dar es
salaam, Askofu Oram Mustafa kutoka Arusha, Mchungaji Titus Mkama wa
Ilala TAG Dar es Salaam, Askofu Dkt Peter Muteba wa Afrika Kusini,
Askofu Dkt Tengu Yoka kutoka Nairobi, Mtume Aaron Timoth wa DRC, na
wenyeji Mtume Onesmo na Mwalimu Lilian Ndegi, ambapo watu walipata muda
wa kutosha kujifunza Neno la Mungu kwa ufasaha na kuombewa na watumishi
wote waliohudumu katika Kongamano hilo.
Living Waters Praise Team, Totoo, Kwaya kutoka Glory Land Arusha, na
kwaya kutoka Nairobi walipata kuhudumu kwenye kongamano hilo, huku pia
King Chavala akiwepo kufanya vitu vyake.
|
Askofu Oram Mustafa kutoka Arusha, Gloryland International Church |
|
Mchungaji Titus Mkama wa Ilala
TAG Dar es Salaam |
|
Askofu Dkt. Peter Muteba, Afrika Kusini |
|
Askofu Dkt. Tengu Yoka kutoka Nairobi |
|
Living Waters Praise Team walipokuwa wakihudumu katika Kongamano hilo |
No comments:
Post a Comment