Social Icons

Saturday, 5 July 2014

HATIMAYE MAHAKAMA SUDAN YAMWACHIA HURU MWANAMKE ALIYETAKIWA KUNYONGWA KWA KUBADILI DINI

Meriam na mumewe Daniel siku ya harusi yao.
Wakili wake Elshareef Ali, ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.
'Hamu kumuona mkewe'
Mumewe Meriam Daniel Wani, alisema kuwa ana hamu sana kumuona mkewe kwani taarifa hiyo ilitolewa bila yeye mwenyewe kuitarajia.
Ameambia BBC kuwa anataka familia yake kuondoka nchini Sudan haraka iwezekanavyo.
Wanandoa hao waliona kanisani baada ya kukutana mwaka 2011.
Mume wa Meriam Daniel Wani akiwa amewapakata watoto wake, mdogo kushoto alizaliwa gerezani hivi karibuni.
Hukumu ya kifo dhidi ya Meriam Yahia Ibrahim Ishag, ambaye alijifungulia gerezani, ilisababisha gadhabu sana hadi katika ulingo wa kimataifa.
"Tuna furaha sana kuhusu hatua hii ya serikalli na tunaelekea sasa kumchukua,'' alisema wakili wa Bi Meriam Elshareef Ali.
Bwana Ali alisema kuwa Bi Meriam alionyesha ujasiri mkubwa sana wakati huu wa masaibu yaliyomkumba.


''Ni ushindi kwa uhuru wa dini na imani, tunaamini kuwa katika siku za usoni hakuna mtu atakayelazimika kupitia masaibu kama yaliyomkumba Meriam,'' alisema wakili wake.
Babake Meriam alikuwa muisilamu ingawa mamake alikuwa mkristo na Meriam akaamua kuolewa na mwanamume mkristo.
Amekuwa gerezani tangu mwezi Februari pamoja na mwanawe mdogo.
Hata hivyo bwana Ali alisema kuwa hajaona hukumu ya mahakama ya rufaa na kwamba alipokea taarifa hizo kupitia kwa vyombo vya habari. BBC Swahili imeripoti

No comments:

Post a Comment