Kanisa la PAG Bukoba lavamiwa,wawili wakatwa mapanga,mmoja afa papo hapo!!
Katika hali isiyo ya kawaida,watu
wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia Kanisa la PAG tawi la
Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na kumua muumini mmoja kwa
kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake kujeruhiwa.hawakuiba chochote
ikiwemo simu zao.
Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo ni wapinzani ya dini yao.
Mwandishi wa mtandao wa harakatinews
amefika katika eneo hilo na kushuhudia sehemu ya madhabahu ikiwa
imetapakaa damu (tazama picha) na imeelezwa na mashuhuda kuwa damu
husika ni wakati marehemu na mwenzake walipokuwa wakitaka kujinusuru
kutoka kwa wakora hao.
Inaelezwa kuwa hadi wanatendewa kitendo
husika walikuwemo peke yao majira ya saa 8 usiku baada ya wenzao
kuondoka katika baada ya ibada usiku kumalizika saa 4 usiku hivyo wao
waliamua kulala kanisani.
Mtoa habari aliyegoma kutaja jina
amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha muumini ambaye ni mwalimu
katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya marehemu kuoa mwanamke wa
dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha dini huyo mkewe na hapo
waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi
mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya pande mbili.
Polisi bado wanachunguza na watatoa
taarifa baadaye,mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha maiti
bukoba mjini,majeruhi amelazwa hospital ya mkoa.
No comments:
Post a Comment