skip to main |
skip to sidebar
Tegemeo langu ni Yesu tu!
Bwana Yesu asifiwe.
Nawasalimu katika jina la Bwana.
Naitwa
Vicky nipo Dar es salaam Tanzania. naomba niwashirikishe hitaji langu
mnisaidie kuomba. Nyumba yangu imekuwa chungu kila siku machozi
yananitoka kwa kukosa amani. Mume wangu ni mlevi ana kauli zinazo umiza
za kejeli na dharau kubwa, tangu amejiunga kwenye Siasa nyumba yangu
imekuwa haina amani tena. Anapenda kunywa sana, amekuwa mtu wa wanawake,
hajali kama ana mke salamu kwake ni nadra sipaswi kuuliza chochote
kutoka kwake nitaambulia maneno ya masimango na dharau. Tena anasema
hata nimuombe vipi Mungu yeye hawezi kubadilika atabadilika atakapo
sijisikia.
Wapendwa naumia sana. Naishi kama
mtumwa, nimekata tamaa. Mume wangu hafanyi kitu chochote bila kwenda
kwa waganga wa kienyeji hata leo hii asubuhi nimekuta kwenye nguo zake
dawa za kienyeji aina tatu, amezifungia kwenye suruali yake. Watu wa
Mungu nisaidieni katika maombi, nitanyanyasika na kudharaulika mpaka
lini. Mimi tegemeo langu ni Mungu tu sina wa kunisaidia wala
wakunisikiliza.
Mungu awabariki.
No comments:
Post a Comment