Mmoja wa mabinti aliyezimia baada ya kumuona mama yake aliyefariki dunia siku nyingi. |
Mchungaji Mwangasa akajaribu kuwatuliza watu kuwa muda wa kibali cha mkutano ulikuwa umeisha ndipo likaibuka lingine baada ya kuwahoji watu hao.
Kumbe, walianguka kutoka hewani ghafla eneo la mkutano, jambo lililowashtua wengi na kuhusu moja kwa moja kuwa ni wachawi. Katikati ya mawazo hayo wakajitokeza mabinti watatu na kusema kuwa yule mwanamke mzee ni mama yao aliyekufa miaka mingi iliyopita. Na mara baada ya kusema hivyo wote wakazimia hapo hapo. Na kuleta kizaazaa kingine.
Umati wa watu ulirindima kwa kelele na fujo na kwa giza hilo ikaonekana si vyema kuendelea na mkutano ndipo ulipoahirishwa na watu kurejea makwao wakitazamia jioni ya leo kusikia ushuhuda kamili.
Mwanaume aliyerudishwa msukule baada ya maombi yaliyofanywa na mchungaji Gwajima kushoto. |
Endelea kuungana nasi ili kupata kilichojiri baada ya hapo... ama tembelea ukurasa wa kanisa la Ufufuo na Uzima
Picha kwa hisani ya Ufufuo na Uzima.MUNGU KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE
No comments:
Post a Comment