Social Icons

Friday, 2 May 2014

EXCLUSSIVE !!MTEKA NYARA AAMUA KUMUACHIA MTOTO BAADA YA KUKERWA NA MTOTO HUYO KUMWIMBIA MUNGU MUDA WOTE


Willie akifanyiwa mahojiano katika moja ya radio huko Atlanta.
Mtoto mvulana wa miaka 10 aitwaye Willie Myrick ametokewa na muujiza mkubwa baada ya kutekwa akiwa nje ya nyumba yao huko Atlanta, Georgia, lakini mda wote akiwa ndani ya gari ya mtekaji huyo, mtoto huyo akapaza sauti kwa Mungu wake na kwakuimba wimbo uitwao 'Every Praise' wa kwake Hezekiah Walker licha ya kukatazwa kuimba hakusikia alizidi kuimba wimbo huo, hivyo mtekaji huyo akaamua kumuachia.

Akizungumza ushuhuda wake kupitia kituo cha runinga cha WXIA-TV Willie amesema alikuwa nje ya nyumba yao ndipo alipotokea mtekaji huyo aliyetaka kumuahadaa kumpa pesa iwapo angeingia
Mchoro wa mtekaji uliotolewa na askari wa Atlanta.
ndani ya gari lake lakini mtoto huyo hakuwa rahisi kushawishika ndipo alipobebwa na kuingizwa garini kitendo kilichomfanya mtoto huyo kuimba wimbo huo wenye maneno kama'God my Saviour, God my Healer, God my Deliverer, Yes He is' mda wa masaa matatu akiwa ndani ya gari hilo licha ya kukatazwa hakusikia kitendo kilichomkera na kuamua kumuachia mtoto huyo huku mtu huyo akimwambia Willie asimwambie yeyote juu ya kitendo hicho.

Kitendo cha mtoto huyo ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi wakati akishuhudia kanisani kwao kilivuta hisia za wengi namna Mungu anavyotenda kazi katika mazingira hata ambayo hayatarajiwi, mtunzi na mwimbaji wa wimbo huo Hezekiah Walker ametaka kumkumbatia mtoto huyo kwa ushuhuda huo mzito. Ambapo kwasasa tayari polisi wa Atlanta wameachia mchoro wa picha ya mtu aliyehusika katika kumteka mtoto Willie, ambaye hushuhuda wake hapana shaka umemtangaza Kristo kwa mara nyingine katika taifa hilo ambalo linapoteza uhalisia wa kuabudu miaka ya karibuni, lakini pia taarifa hizi zimeendelea kuenea katika vyombo mbalimbali duniani ikiwemo gazeti la METRO la London Uingereza ambalo pia liliandika habari hii.

                         Taarifa za Willie na ushuhuda wake ndani ya vyombo vya habari.


       Tazama wimbo uliomfanya mtekaji kumuachia mtoto Willie, kama hukupata kuufahamu.

No comments:

Post a Comment