Wiki iliyopita tulitazama miongozo michache inyoweza kukusaidia maishani
mwako, na hiyo ni pamoja na kuepuka kuongea matatizo yako mara kwa
mara, kuongea baraka na tumaini kwa maisha ya wengine, na kadhalika,
bofya hapa kusoma.
Faraja Naftal Mndeme |
Leo tutajifunza mambo machache yanayoweza kuongeza thamani katika
mahusiano yako ya aina yoyote ile kati ya watu wawili au zaidi.
1. Jiandae kupoteza zaidi kuliko kupata zaidi.
Mara nyingi tumekuwa mahusiano ambayo huwa tunatarajia kupata zaidi ya kupoteza.Kiukweli kabla hujakuwa na mahusiano yoyote au tayari unayo tambua kupoteza ni zaidi kuliko kupata.Kumbuka unapoingia kwenye mahusiano yoyote tayari ulishakuwa na mfumo wako binafsi uliozoea wa maisha,tabia zako,ratiba zako lakini linapokuja swala la watu wawili au zaidi ujue kuna mambo mengi yatakufa ili kutengeneza kitu kimoja ambacho hakitakuwa cha umimi wala yule kinakuwa chenu.Ukiingia kwenye mahusiano yoyote ukitarajia kuwa na furaha zaidi ya kuipoteza ujue huo uhusiano utakusmbua sana au hakuna mahusiano yoyote yatakayodumu maishani mwako.Mahusiano yoyote ni Win Win Situation sio kila jambo ushinde au kunonekana mbabe zaidi ya wenzako.
2. Jiandae Kisaikolojia.
Iwapo tangu mwanzo wa mahusiano yako na watu wengine haukujianda kisaikolojia juu ya changamoto na matatizo ambayo unaweza kukutana nayo na kuyatatua,ujue mahusiano hayo yatakufa tu hata kama yatakuwepo basi ya kulega lega.Kwa asili kila binadamu ana mapungufu yake ya asili ambayo mara nyingi huwezi kuyaona moja kwa moja na hata kama utayaona ujue ni kwa sehemu tu.Jua kuna mengi yapo nyuma ya pazia ambayo hukuweza kuyajua au kuyafikiria.Ni muhimu kujua kila mtu kwa asili ana hulka na tabia zake tusizozijua.Inakupasa kichwa chako
Kiwe empty na flexible kwa aina yeyote situation inayoweza tokea.Mahusiano yoyote kumbuka yanahusisha binadamu na sio malaika.
3. Tarajia yasio Tarajiwa.
Maisha huwa yana surprise nyingi ambazo hatuzitaraji vile vile mahusiano yoyote ni sehemu ya maisha.Unaweza kukuta wakati mahusiano yanaanzishwa watu walikuwa na ambitions nyingi sana ambazo badae zinaweza kubadilika kulingana na wakati pia kuna mabadiliko ambayo ya asili mtu huyapitia mfano Wakati mtu mwingine akiwa na Stress hawezi ongea kabisa na wakati wewe umemzoea ni muongeaji sana.Mwingine akikasirika huwasilisiani na wengine mpaka muda fulani upite.Ni muhimu kuyatarajia yasiyo tarajika chochote chaweza tokea kwa maana mifumo ya vichwa na bongo zetu zinavyoprocess information zimetofautiani kulingana na mazingira na wakati pia.
4. Anger Management & Stress Management.
Binadamu tunapitia vipindi mbali mbali vya maisha vingine huwa vigumu
zaidi ambavyo husababisha misongo ya mawazo.Ni muhimu sana kujua na
kujifunza namna ya kutatua tatizo la Misongo ya mawazo inayotukabili
kila siku.Siku hizi kuna Online courses za namna ya kutatua na kudhibiti
misongo ya mawazo chukua muda kujifunza na kutendea kazi.
Anger Management ni kitu muhimu sana kujifunza maana jambo lolote linalohusisha watu zaidi ya mtu mmoja ujue lazima kunatakuwa kutakuwa na migongano ya mawazo ni muhimu sana sana kujifunza na kidhibiti maamuzi yasababishwayo na hasira.
Ukiwa na hasira bila namna ya kujua kuzidhibiti itakupelekea kuwa na stress ambazo zitapelekea kichwa chako kufikiria kwa kiwango cha chini.Ukishindwa kuwa na Anger & Stress Management kila mara hakuna mahusiano yako yoyote yatakayodumu.
5. Ability to Solve Conflicts (Uwezo wa kutatua na Kuvuka Changamoto/Migogoro)
Ni muhimu kuzijua changamoto zilizo kwenye mahusiano yoyote pia na njia za utatuzi wa changamoto hizi.Kila mahusiano yana changamoto zake lakini utatuzi haufwanani.Ni muhimu kuwa na mbinu mbadala na uwezo wa kujua changamoto itakayojitokeza inahitaji ni kitu gani na pia ni wakati gani.Mbinu za utatuzi zinaweza kuwa sahihi lakini mahali na muda zilipotumika sio sahihi.Kwa namna hiii mahusiano hayo hayawezi kudumu bali yatakuwa ya kuegesha.Ni muhimu sana kuendelea kujifunza na kuongeza uwezo wa zaidi na zaidi wa namna ya utatuzi wa migogoro na changamoto za kwenye mahusiano.
6. Mahusiano yoyote yanapaswa kujengwa kwenye Neno la Mungu.
Iwapo wewe ni mkristo/dini nyingine ni muhimu kujua kwanza mahusiano ya mwanadamu na muumba wake kiundani zaidi kuliko kukariri.Unaweza ukawa unasoma vizuri vitabu vya dini lakini namna ya kuelewa hamusiano yaliopo kati ya Mwanadamu na Muumba wako ni ngumu.Imekupasa kuelewa every single detail ya mahusiano kati yako na Muumba wako.Pia uzuri vitabu vingj vya dini vimejaribu kuonyesha migogoro ya kimahusiano na utatuzi wake ulivyopatikana.Ni muhimu kuelewa na kutendea kazi kuliko kukariri.Mungu ndie muasisi wa mahusiano yoyote unayoyaona leo na hata yatakayo kuwepo kesho.
No comments:
Post a Comment