Haya msomaji wetu wa Gospel is hot karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka
comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Mji wa Ninawi uonekanavyo kwasasa. |
KWA TAARIFA YAKO hii leo
tumeamua kukujulisha moja ya mji ambao upo mpaka leo, habari zake
zimeandikwa kwenye Biblia. Kama umesoma kitabu cha Yona katika Biblia
utakutana na mji uitwao Ninawi ambao nabii Yona alitumwa na Mungu kwenda
kuwahubiria habari njema lakini yeye akakwepa jukumu alilopewa na Mungu
na kuamua kukimbilia Tarishishi, lakini kwakuwa Mungu hakimbiwi
misukomisuko aliyoipata aliamua kujisalimisha kwa Mungu na kuitikia wito
wa kwenda Ninawi kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Yona 3
KWA TAARIFA YAKO mji wa Ninawi upo mashariki ya kati nchini Iraki. Mji huo unaoaminika kukaliwa na Wakristo wengi upo kilometa 400 kaskazini magharibi mwa Iraki, ingawa toka vita ilipoingia ya kumuondoa aliyekuwa Rais wa nchi ya Iraki marehemu Saddam Hussein, inaelezwa idadi ya Wakristo katika mji huo imepungua kwasababu baada ya mji mkuu wa Mosul kutekwa na waislamu wenye msimamo mkali wanaojiita Islamic state ama Isis zamani wakitambulika hivyo, kumewafanya wakristo wengi kuukimbia mji wa Mosul ambao majengo yake ni ya kisasa zaidi kulinganisha na Ninawi.
KWA TAARIFA YAKO kwa
mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) katika taarifa yake
ya habari hivi karibuni lilitangaza kwamba namba ya wakristo imeshuka
kutoka milioni 1 na laki tano mwaka 2003 mpaka 350,000 - 450,000, ambapo
wengi wao waliobakia wanaishi vijijini kama kijiji cha Qaraqosh ambacho
pia kinafahamika kwa jina lingine kama Baghidada, Bartella,
Al-Hamdaniya pamoja na Tel Kef ambavyo vipo ndani ya Ninawi.
KWA TAARIFA YAKO mwishoni mwa wiki iliyopita wakristo waliamliwa kuondoka katika mji wa Mosul, tamko lililotolewa na wanajeshi wa Sunni (moja ya majeshi makubwa ya kiislamu) na mpaka kufikia jumamosi iliyopita wakristo wengi waliamua kuhama mji huo na kukimbilia miji ya karibu inayokaliwa na wakristo, kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari vya kimataifa vinasema wakristo waliamua kuondoka Mosul wakiacha samani zao nyuma na kuondoka na nguo walizovaa tu na kukimbilia kijiji cha Al Qosh mji mkubwa wa wakristo ambao unadaiwa kabla majeshi hayo ya kiislamu kuchukua mji ulikuwa na wakristo wafikao 30,000 lakini toka june mwaka huu wakristo waliosalia waliamua kuukimbia mji. (Popote ulipo maombi yako ni muhimu sana kwa ndugu zetu hawa).
KWA TAARIFA YAKO tukio kubwa kuwahi kutokea katika nchi ya Iraki
dhidi ya Wakristo ilikuwa mwaka 2010 wakati watu 52 walipoteza maisha
mara baada watu wasiofahamika kujitoa muhanga ndani ya kanisa mjini
Baghdad siku ya jumapili wakati wakristo wakiwa ibadani. KWA TAARIFA YAKO hayo ndiyo tuliyokuandalia hii leo japo kwa ufupi lakini pia KWA TAARIFA YAKO
unakumbuka habari ya mnara wa Babeli? hivi unajua nao mji wake upo
nchini Iraki? kwa leo tunaishia hapa, tukutane tena wiuki ijayo.. Mungu
akubariki
Yona 3
1 Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema,
2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.
3 Basi
Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi
ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu.
4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.
5 Basi
watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo
za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.
6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua
Ramani inayoonyesha mji wa Ninawi ulipo. |
vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
7 Naye
akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya
mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala
makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;
8 bali
na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie
Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na
udhalimu ulio mikononi mwake.
9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?
10 Mungu
akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu
akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
KWA TAARIFA YAKO mji wa Ninawi upo mashariki ya kati nchini Iraki. Mji huo unaoaminika kukaliwa na Wakristo wengi upo kilometa 400 kaskazini magharibi mwa Iraki, ingawa toka vita ilipoingia ya kumuondoa aliyekuwa Rais wa nchi ya Iraki marehemu Saddam Hussein, inaelezwa idadi ya Wakristo katika mji huo imepungua kwasababu baada ya mji mkuu wa Mosul kutekwa na waislamu wenye msimamo mkali wanaojiita Islamic state ama Isis zamani wakitambulika hivyo, kumewafanya wakristo wengi kuukimbia mji wa Mosul ambao majengo yake ni ya kisasa zaidi kulinganisha na Ninawi.
Watoto wakicheza nje ya nyumba zao huko Ninawi©nationalgeographical. |
KWA TAARIFA YAKO mwishoni mwa wiki iliyopita wakristo waliamliwa kuondoka katika mji wa Mosul, tamko lililotolewa na wanajeshi wa Sunni (moja ya majeshi makubwa ya kiislamu) na mpaka kufikia jumamosi iliyopita wakristo wengi waliamua kuhama mji huo na kukimbilia miji ya karibu inayokaliwa na wakristo, kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari vya kimataifa vinasema wakristo waliamua kuondoka Mosul wakiacha samani zao nyuma na kuondoka na nguo walizovaa tu na kukimbilia kijiji cha Al Qosh mji mkubwa wa wakristo ambao unadaiwa kabla majeshi hayo ya kiislamu kuchukua mji ulikuwa na wakristo wafikao 30,000 lakini toka june mwaka huu wakristo waliosalia waliamua kuukimbia mji. (Popote ulipo maombi yako ni muhimu sana kwa ndugu zetu hawa).
Lango la kuingilia mji wa Ninawi lionekanavyo kwasasa©atlastours. |
No comments:
Post a Comment