Askofu mkuu Zachary Kakobe. |
Katika mistari hii, tunaona juu ya ndugu zake Yesu Kristo. Kuna umuhimu wa kujifunza kwa undani juu ya somo hili. Tutaligawa somo letu, katika vipengele viwili:-
1. NDUGU WA KIMWILI WA YESU KRISTO;
2. NDUGU WA KIROHO WA YESU KRISTO.
(1) NDUGU WA KIMWILI WA YESU KRISTO
Katika MATENDO 19:23-28, tunaona habari za mungu mke Artemi ambaye alikuwa anaabudiwa Asia yote na sehemu nyingi za ulimwengu. Hali hii ya watu kuabudu mungu mke ilisambaa sana hata karne zilizofuata katika sehemu nyingi za ulimwengu. Katika upagani huo, mungu huyo mke, alisemekana kwamba ni bikira aliyekuwa na mtoto mmoja tu ambaye yeye pia alikuwa na sifa za uungu. Wakati wote, sanamu za mungu huyo mke zilionyesha mwanamke aliyekuwa na mtoto wa kiume mikononi. Sehemu mbalimbali ulimwenguni, mungu huyo mke alikuwa na majina tofauti – Misri walimwita jina “ISIS“, India walimpa jina “ISI“, sehemu kadha za Asia walimwita “CERES“, China nao walimwita “SHING MOO“ n.k.
Hatimaye, upagani huu, ulipenya katika Kanisa na ikazuliwa kuwa Bikira Mariamu ana sifa za Uungu, ni mama yake Mungu (kinyume kabisa na maandiko yanavyotaja kwamba ni mjakazi wa Bwana – LUKA 1:38). Ikazuliwa pia kwamba:
Mariamu mama yake Yesu hakuwa na watoto wengine, eti ndugu zake Yesu .
SABABU NNE ZINAZOTHIBITISHA KWAMBA MARIAMU ALIZAA
(a) Wanaotajwa, walikuwa binamu zake Yesu kwa Mariamu mwingine;
(b) Yusufu alikuwa mzee sana kuwa na watoto kwa Mariamu mama yake Yesu;
(c) Yusufu alikuwa na watoto kwa mke mwingine aliyemwoa kabla ya Mariamu na eti pia kwamba Mariamu aliendelea kuwa Bikira wakati wote.
Yote haya yalikuwa na lengo la kulifanya Kanisa liingizwe katika ibada za kipagani za mungu mke. Ni huzuni kwamba uzushi huu bado umeendelea kushikiliwa na watu wengine ulimwenguni wajiitao “Wakristo“. Kama wanafunzi wa Biblia, ni muhimu kuijua kweli juu ya jambo hili.
WATOTO WENGINE BAADA YA KUMZAA YESU
Ilitabiriwa kwamba Masihi (Yesu Kristo) atakuwa mgeni kwa ndugu zake na wana wa mama yake (ZABURI 69:8-9). Linganisha utabiri huu na YOHANA 7:1-9; 2:3-17;
Akamzaa mwanawe kifungua mimba (LUKA 2:6-7). Neno hili “kifungua mimba“ kwa Kiyunani, linajulikana kama “PROTOTOKOS“, na kila linapotumika katika Biblia, linaelezea maana ya “WA KWANZA MIONGONI MWA WENGI“. Neno hili linatumika katika WARUMI 8:29; WAKOLOSAI 1:15, 18; UFUNUO 1:5. Kama Yesu anagekuwa mwana pekee kwa Mariamu, Neno la Kiyunani, “MONOGENES“ ndilo ambalo lingetumika. Neno hili linapotumika katika Biblia, linamaanisha “MWANA PEKEE BILA YEYOTE MWINGINE KUMFUATA“. Neno hili linatumika kuzungumzia mwana pekee wa Mwanadamu (LUKA 7:12; LUKA 8:42; LUKA 9:38) na mwana pekee wa Mungu (YOHANA 1:14, 18; 3:16, 18; 1 YOHANA 4:9).
Inatajwa waziwazi kwamba Yesu alikuwa na ndugu wa kiume wanne na dada zake pia (maumbu) – MATHAYO 13:55-56; MARKO 6:1-3; WAGALATIA 1:18-19).
Inatajwa kwamba mama yake Yesu na ndugu zake, walimfuata Yesu wakitaka kusema naye (MATHAYO 12:46-47; MARKO 3:31-32).
Mariamu, mama yake Yesu, alikuwa mmoja tu kati ya wanafunzi wa Yesu 120 walioketi orofani kumwomba Mungu kwa ajili ya ahadi ya Roho Mtakatifu. Hakuwa na tofauti, na hata sasa hana tofauti yoyote na mwanafunzi yeyote wa Yesu (MATENDO 1:12-15). Yeye alimwomba Mungu, sisi nasi tunamwomba Mungu kwa Jina la Yesu kama yeye. Mariamu alikuwa mmoja tu kati ya mabikira wengi wa nyakati hizo za Biblia (MWANZO 24:15-16; ESTA 2:2-4; EZEKIELI 44:22; MATENDO 21:9). Miongoni mwa mabikira wengi, Mariamu alipata neema na kibali mbele ya Mfalme Ahasuero, kuliko mabikira wote waliokuwepo (ESTA 2:2-4, 17; linganisha na LUKA 1:30-31).
2. NDUGU WA KIROHO WA YESU KRISTO (MATHAYO 12:48-50; MARKO 3:33- 35)
Yesu Kristo, alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo, mtu anapozaliwa mara ya pili, anazaliwa kwa Roho Mtakatifu (YOHANA 3:3-6; TITO 3:4-5). Kwa sababu hiyo mtu aliyezaliwa mara ya pili, anakuwa ndugu yake Yesu Kristo. Yesu kwa njia hii, amekuwa mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi (WARUMI 8:29; WAEBRANIA 2:11-12). Yesu Kristo ni kaka yetu wa kwanza! Mahali hapa tunapata fundisho kubwa:-
Katika familia, inapotokea kwamba mtoto wa kwanza kuzaliwa ni wa kiume, huyo anakuwa bwana wa ndugu zake wote (MWANZO 27:29). Ndugu wengine wote wanamtegemea kaka yao na kaka huyo anawajibika kuwasaidia nduguze. Yesu Kristo kama kaka yetu, anawajibika kutusaidia na anatuambia, “OMBENI NANYI MTAPEWA“.
Ndugu katika familia mara kwa mara hufanana. Inabidi wakati wote tuonyeshe kufanana na Yesu Kristo ikiwa kweli tuna undugu naye (WAGALATIA 6:1-7). Ni muhimu sana kuhakikisha kwamba tunautunza ushuhuda wetu wa kufanana na Yesu kila mahali, kazini, nyumbani, na popote pale. Ushuhuda wa wokovu wetu, ni wa thamani sana kwa kuifanya Injili iwafikie watu wote kwa mafanikio. Doa dogo katika ushuhuda wetu, linaifanya Injili iwe vigumu kuwafikia watu wengine.
Maandiko yanatufundisha wazi kwamba ndugu zake Yesu ni wale tu wanaoyafanya Mapenzi ya Mungu (MATHAYO 12:50; MARKO 3:35). Hatuwezi kudai kwamba Yesu ni ndugu yetu ikiwa hatufanyi sawasawa na Neno la Mungu. Tunasikia, lakini hatutendi. Heri yeye anayesikia maneno ya Mungu na kuyafanya. Huyo ni mtu mwenye akili, ni ndugu yake Yesu, ni mtoto wa Mungu, ni mwana wa Mungu (MATHAYO 7:24-27).
UTUNZE USHUHUDA WAKO, DUMU KUWA MTOTO WA MUNGU.
Unaweza kuingia katika somo “UMUHIMU WA KUWA NA HEKIMA” katika link hiihttp://davidcarol719.wordpress.com/umuhimu-wa-kuwa-na-hekima/
…………………………………………………………………………………………………………………………………..
Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!
Neno la Uzima Kutoka Kwa Askofu Mkuu Zachary Kakobe
Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org
Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries
Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobea.
Zinazohusiana

Comments/disqusion
No comments