Kwaya maarufu Afrika mashariki na kati ya Ambassadors of Christ ya jijini Kigali nchini Rwanda hapo jana imefanya huduma kubwa ya kuwapikia chakula wagonjwa wasiokuwa na ndugu wanaopatiwa matibabu katika hospitali kubwa nchini humo iitwayo University hospital.
Kwa mujibu wa maelezo waliyotoa kwaya hiyo kupitia ukurasa wao wa Facebook wameeleza kwamba kufanya kwao hivyo ni kutimiza andiko kuhusu dini iliyosafi ambapo wakanukuu Matayo 25:35-36 Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula; nilikuwa na kiu mkanipa kitu cha kunywa; nilikuwa mgeni mkanikaribisha; 36 nilikuwa sina nguo, mkanivisha; nilikuwa mgonjwa mkaja kunitazama; na nilikuwa kifungoni mkaja kunitembe lea.’ 37 “Kisha wale wenye haki watamjibu, ‘Bwana, ni lini tuli kuona na njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakupa kitu cha kunywa ? 38 Na ni lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukihitaji nguo tukakuvisha? 39 Na ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’
40 “Mfalme atajibu, ‘Ninawaambia kweli, kwa jinsi ambavyo mlivyomfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlini fanyia mimi.
Wanakwaya wa Ambassadors kwa pamoja walipika chakula hicho kisha kuwahudumia wagonjwa hao ambao kwa pamoja walionekana wenye sura za matumaini na shukrani kwa kwaya hiyo ambayo inakubalika sana nchini Rwanda.
No comments:
Post a Comment