Social Icons

Featured Posts

Sunday, 12 October 2014

Kanisa la PAG Bukoba lavamiwa,wawili wakatwa mapanga,mmoja afa papo hapo!!


Katika hali isiyo ya kawaida,watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia Kanisa la PAG tawi la Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na kumua muumini mmoja kwa kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake kujeruhiwa.hawakuiba chochote ikiwemo simu zao.

Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo ni wapinzani ya dini yao.

Mwandishi wa mtandao wa harakatinews amefika katika eneo hilo na kushuhudia sehemu ya madhabahu ikiwa imetapakaa damu (tazama picha) na imeelezwa na mashuhuda kuwa damu husika ni wakati marehemu na mwenzake walipokuwa wakitaka kujinusuru kutoka kwa wakora hao.

Inaelezwa kuwa hadi wanatendewa kitendo husika walikuwemo peke yao majira ya saa 8 usiku baada ya wenzao kuondoka katika baada ya ibada usiku kumalizika saa 4 usiku hivyo wao waliamua kulala kanisani.


Mtoa habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha dini huyo mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya pande mbili.

Polisi bado wanachunguza na watatoa taarifa baadaye,mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha maiti bukoba mjini,majeruhi amelazwa hospital ya mkoa.

Viongozi wa makanisa ya PAG watatoa tamko .


Saturday, 27 September 2014

Usiyaone matatizo ya kiuchumi kama Kikwazo – Mwl Mwakasege

mwakasege

Shalom,

Tunajua unataka uwe na uchumi mzuri. Hii ni kwa mwanadamu yeyote bila kujali mahali alipo,awe anafanya kazi au hata kama hafanyi kazi.

Kuanzia leo na siku kadhaa zitakazofuata,tutajitahidi kukushirikisha misingi kadhaa iliyomo katika biblia,ambayo tunaamini itakusaidia uwe na uchumi mzuri. Msingi wa kwanza ni huu:Badilika unavyoamini juu ya uchumi,utabadilika unvyosema juu ya uchumi,na hali yako ya uchumi itabadilika vivyo hivyo.

Tunaamini ya kuwa; mtu akibadilika anavyoamini atabadilika pia anavyosema;na hali yake ya maisha itabadilika vivyo hivyo.

MUNGU AWEZA KURUDISHA NDOA ZILIZOKUFA SOMA HII ITAKUSAIDIA WEWE MWANANDOA

Tumeona ndoa nyingi za watumishi wa Mungu zikivunjika au zikiwa katika hati-hati ya kuvunjika kutokana na sababu mbali mbali, ndoa zote zilizo hoi zinahitaji dawa ambayo ni Bwana Yesu!

Karibuni tulishuhudia ndoa ya mtumishi wa Mungu maarufu duniani Benn Hinn Kurejeshwa baada ya kuachana na mkewe kwa muda,

VIDEO!BAADA YA WAUMINI KULISHWA MAJANI NA NABII SASA AWANYWESHA PETROLI...

Wakati kitendo cha kuwaambia waumini wake kula majani pamoja na kusimama juu yao huku akiwafanyia maombi  bado vikiwa vimewapiga butwaa watu wengi duniani, nabii Lesego Daniel wa huduma ya Rabboni Ministries iliyopo nchini Afrika ya kusini, sasa anawanywesha waumini wake mafuta ya petroli ambayo anadai ameyaombea na kugeuka kuwa juisi ya mananasi.

Katika video iliyopo chini utaweza kujionea kwa kina namna waumini wanavyogombea kunywa petroli (kama inavyosemekana) na kutoa shuhuda kwamba ina ladha nzuri kama juisi ya mananasi huku wengine wakimuomba nabii na profesa Lesego Daniel awaongeze juisi hiyo.

Wednesday, 24 September 2014

EXCLUSSIVE SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WANANCHI WAKE KWENDA KWA TB JOSHUA NIGERIA

Kanisa la Mtume TB Joshua kabla ya kuanguka.



Waziri Henri Eyebe Ayissi 

Mtume TB Joshua akikagua zoezi la uokoaji kanisani kwake.

Wakati vyombo vya habari vya kimataifa vikiripoti watu 115 wamefariki dunia kutokana na kuanguka kwa kanisa la mtume TB Joshua wa Nigeria la Church of All Nations, serikali ya Cameroon imewapiga marufuku wananchi wake kwenda kanisani au kujihusisha na mtume huyo ikidai kwamba ni wakala wa shetani na kwamba amekuwa akiudanganya umma kupitia miujiza waliyoiita ya kishetani.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nje na mahusiano wa Cameroon mheshimiwa Henri Eyebe Ayissi katika waraka wake alioutoa mapema wiki iliyopita ukiwa na kichwa cha habari kisemacho 'shetani yupo ndani ya nyumba' akimaanisha mtume TB Joshua kwa kumuita mtoto wa shetani akijofanya ni mtumishi wa Mungu.

Waziri huyo amewaonya mamia ya wananchi wa Cameroon wanaokwenda kusini magharibi mwa jiji 

Thursday, 4 September 2014

MISTARI 7 YA BIBLIA KUKUINUA KWENYE SIKU MBAYA


Habari yako? Siko yako ama ya rafiki yako inaendaje? Kama basi uko vibaya na unahisi mambo yamekuelemea, ama hata rafiki yako, si vibaya kuigeukia Biblia, maana ni kitabu ambacho kwetu sisi Wakristo, kinaonyesha njia. Mistari yake ina uwezo wa kukubadili na kukufariji pia.

Hivyo basi kama wewe ama rafiki yako amekuwa na siku mbaya, pitia mistari hii na uitafakari ahadi ya Mungu kwako. John Calahan wa Christian Post amezikusanya.

1 Petro 5:6-7
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

2 Thesalonike 3:16
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

Wafilipi 4:6-7
Msijisumbu kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Zaburi 50:15
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza

Mathayo 7:7
Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa

1 Thesalonike 5:16-18
Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Tags: Biblia, Neno.
Habari yako? Siko yako ama ya rafiki yako inaendaje? Kama basi uko vibaya na unahisi mambo yamekuelemea, ama hata rafiki yako, si vibaya kuigeukia Biblia, maana ni kitabu ambacho kwetu sisi Wakristo, kinaonyesha njia. Mistari yake ina uwezo wa kukubadili na kukufariji pia.
Hivyo basi kama wewe ama rafiki yako amekuwa na siku mbaya, pitia mistari hii na uitafakari ahadi ya Mungu kwako. John Calahan wa Christian Post amezikusanya.
1 Petro 5:6-7
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
2 Thesalonike 3:16
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.
Wafilipi 4:6-7
Msijisumbu kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Zaburi 50:15
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza
Mathayo 7:7
Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa
1 Thesalonike 5:16-18
Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Comments/disqusion
No comments


- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/09/mistari-7-ya-biblia-kukuinua-kwenye.html#sthash.VtwNRIyb.dpuf

Tuesday, 2 September 2014

TWENDE PAMOJA TUANGALIE JUU YA NDUGU ZAKE YESU......KUMBE YESU ALIKUWA NA NDUGU????????



 
Katika mistari hii, tunaona juu ya ndugu zake Yesu Kristo. Kuna umuhimu wa kujifunza kwa undani juu ya somo hili. Tutaligawa somo letu, katika vipengele viwili:-
1. NDUGU WA KIMWILI WA YESU KRISTO;
2. NDUGU WA KIROHO WA YESU KRISTO.

(1) NDUGU WA KIMWILI WA YESU KRISTO

Katika MATENDO 19:23-28, tunaona habari za mungu mke Artemi ambaye alikuwa anaabudiwa Asia yote na sehemu nyingi za ulimwengu. Hali hii ya watu kuabudu mungu mke ilisambaa sana hata karne zilizofuata katika sehemu nyingi za ulimwengu. Katika upagani huo, mungu huyo mke, alisemekana kwamba ni bikira aliyekuwa na mtoto mmoja tu ambaye yeye pia alikuwa na sifa za uungu. Wakati wote, sanamu za mungu huyo mke zilionyesha mwanamke aliyekuwa na mtoto wa kiume mikononi. Sehemu mbalimbali ulimwenguni, mungu huyo mke alikuwa na majina tofauti – Misri walimwita jina “ISIS“, India walimpa jina “ISI“, sehemu kadha za Asia walimwita “CERES“, China nao walimwita “SHING MOO“ n.k.

Hatimaye, upagani huu, ulipenya katika Kanisa na ikazuliwa kuwa Bikira Mariamu ana sifa za Uungu, ni mama yake Mungu (kinyume kabisa na maandiko yanavyotaja kwamba ni mjakazi wa Bwana – LUKA 1:38). Ikazuliwa pia kwamba:

Mariamu mama yake Yesu hakuwa na watoto wengine, eti ndugu zake Yesu .

SABABU NNE ZINAZOTHIBITISHA KWAMBA MARIAMU ALIZAA

(a) Wanaotajwa, walikuwa binamu zake Yesu kwa Mariamu mwingine;

(b) Yusufu alikuwa mzee sana kuwa na watoto kwa Mariamu mama yake Yesu;

(c) Yusufu alikuwa na watoto kwa mke mwingine aliyemwoa kabla ya Mariamu na eti pia kwamba Mariamu aliendelea kuwa Bikira wakati wote.

Yote haya yalikuwa na lengo la kulifanya Kanisa liingizwe katika ibada za kipagani za mungu mke. Ni huzuni kwamba uzushi huu bado umeendelea kushikiliwa na watu wengine ulimwenguni wajiitao “Wakristo“. Kama wanafunzi wa Biblia, ni muhimu kuijua kweli juu ya jambo hili.

WATOTO WENGINE BAADA YA KUMZAA YESU
Ilitabiriwa kwamba Masihi (Yesu Kristo) atakuwa mgeni kwa ndugu zake na wana wa mama yake (ZABURI 69:8-9). Linganisha utabiri huu na YOHANA 7:1-9; 2:3-17;
Akamzaa mwanawe kifungua mimba (LUKA 2:6-7). Neno hili “kifungua mimba“ kwa Kiyunani, linajulikana kama “PROTOTOKOS“, na kila linapotumika katika Biblia, linaelezea maana ya “WA KWANZA MIONGONI MWA WENGI“. Neno hili linatumika katika WARUMI 8:29; WAKOLOSAI 1:15, 18; UFUNUO 1:5. Kama Yesu anagekuwa mwana pekee kwa Mariamu, Neno la Kiyunani, “MONOGENES“ ndilo ambalo lingetumika. Neno hili linapotumika katika Biblia, linamaanisha “MWANA PEKEE BILA YEYOTE MWINGINE KUMFUATA“. Neno hili linatumika kuzungumzia mwana pekee wa Mwanadamu (LUKA 7:12; LUKA 8:42; LUKA 9:38) na mwana pekee wa Mungu (YOHANA 1:14, 18; 3:16, 18; 1 YOHANA 4:9).
Inatajwa waziwazi kwamba Yesu alikuwa na ndugu wa kiume wanne na dada zake pia (maumbu) – MATHAYO 13:55-56; MARKO 6:1-3; WAGALATIA 1:18-19).
Inatajwa kwamba mama yake Yesu na ndugu zake, walimfuata Yesu wakitaka kusema naye (MATHAYO 12:46-47; MARKO 3:31-32).

Mariamu, mama yake Yesu, alikuwa mmoja tu kati ya wanafunzi wa Yesu 120 walioketi orofani kumwomba Mungu kwa ajili ya ahadi ya Roho Mtakatifu. Hakuwa na tofauti, na hata sasa hana tofauti yoyote na mwanafunzi yeyote wa Yesu (MATENDO 1:12-15). Yeye alimwomba Mungu, sisi nasi tunamwomba Mungu kwa Jina la Yesu kama yeye. Mariamu alikuwa mmoja tu kati ya mabikira wengi wa nyakati hizo za Biblia (MWANZO 24:15-16; ESTA 2:2-4; EZEKIELI 44:22; MATENDO 21:9). Miongoni mwa mabikira wengi, Mariamu alipata neema na kibali mbele ya Mfalme Ahasuero, kuliko mabikira wote waliokuwepo (ESTA 2:2-4, 17; linganisha na LUKA 1:30-31).

2. NDUGU WA KIROHO WA YESU KRISTO (MATHAYO 12:48-50; MARKO 3:33- 35)

Yesu Kristo, alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo, mtu anapozaliwa mara ya pili, anazaliwa kwa Roho Mtakatifu (YOHANA 3:3-6; TITO 3:4-5). Kwa sababu hiyo mtu aliyezaliwa mara ya pili, anakuwa ndugu yake Yesu Kristo. Yesu kwa njia hii, amekuwa mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi (WARUMI 8:29; WAEBRANIA 2:11-12). Yesu Kristo ni kaka yetu wa kwanza! Mahali hapa tunapata fundisho kubwa:-
Katika familia, inapotokea kwamba mtoto wa kwanza kuzaliwa ni wa kiume, huyo anakuwa bwana wa ndugu zake wote (MWANZO 27:29). Ndugu wengine wote wanamtegemea kaka yao na kaka huyo anawajibika kuwasaidia nduguze. Yesu Kristo kama kaka yetu, anawajibika kutusaidia na anatuambia, “OMBENI NANYI MTAPEWA“.
Ndugu katika familia mara kwa mara hufanana. Inabidi wakati wote tuonyeshe kufanana na Yesu Kristo ikiwa kweli tuna undugu naye (WAGALATIA 6:1-7). Ni muhimu sana kuhakikisha kwamba tunautunza ushuhuda wetu wa kufanana na Yesu kila mahali, kazini, nyumbani, na popote pale. Ushuhuda wa wokovu wetu, ni wa thamani sana kwa kuifanya Injili iwafikie watu wote kwa mafanikio. Doa dogo katika ushuhuda wetu, linaifanya Injili iwe vigumu kuwafikia watu wengine.
Maandiko yanatufundisha wazi kwamba ndugu zake Yesu ni wale tu wanaoyafanya Mapenzi ya Mungu (MATHAYO 12:50; MARKO 3:35). Hatuwezi kudai kwamba Yesu ni ndugu yetu ikiwa hatufanyi sawasawa na Neno la Mungu. Tunasikia, lakini hatutendi. Heri yeye anayesikia maneno ya Mungu na kuyafanya. Huyo ni mtu mwenye akili, ni ndugu yake Yesu, ni mtoto wa Mungu, ni mwana wa Mungu (MATHAYO 7:24-27).

UTUNZE USHUHUDA WAKO, DUMU KUWA MTOTO WA MUNGU.


Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa