Kifungo ©Stand up for the truth |
Taarifa mpya ya utafiti imeanika wazi kwamba taifa la Nigeria ndio nchi ambayo wakristo
nchini humo wanaishi kwa mateso makubwa, ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la Open Doors kupitia kitengo
chake cha World Watch List kuanzia kipindi cha November 1, 2012 hadi Machi 31, 2014,
Nigeria imeshika namba moja ikifuatiwa na mataifa ya Syria, Misri, Jamhuri ya Afrika
ya Kati, Mexico, Pakistan, Colombia, India, Kenya na Iraq.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo imeegemea takwimu za namna makanisa na
mali za wakristo zilivyoteketezwa, na maasi dhidi yao mathalani kupigwa,
utekwaji nyara, ubakaji, kukamatwa hovyo na hata kulazimishwa ndoa, inaonyesha
kuwa Nigeria inaongoza ikiwa na matukio 2,073 huku Syria ikiwa na matukio
1,479. Mataifa mengine yanayofuatia ni pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati
1,115, Pakistan 228, Misri 147, Kenya 85, Iraq 84, Mnyanmar (Burma) na Sudan
ikiripotiwa kuw ana 33, na Venezuela ikiwa na matukio 26.
"Kujitangaza kwamba ni mkristo kwenye mataifa haya ni kama kujitoa
mhanga, unajiweka hatarini"
Na kati ya mauaji 5,479 ya wakristo duniani kote, Nigeria, Syria na Jamhuri ya
Afrika ya Kati wameunda asilimia 85 ya jumla hiyo, huku takwimu zikikadiria
kuwa kuna wakristo 322 wanaouwawa kila mwezi.
Korea ya Kaskazini, taifa ambalo linaongoza kwa mateso ya wakristo kwa mwaka
2014, halijaorodheshwa kwenye 'kumi bora' kutokana na kinachoendelea nchini
humo kuwa cha siri mno kiasi kwamba unaweza usijue kilichopo, kulinganisha na
muundo wa utafiti huo ambao umebeza taarifa za mitandao, vyombo vya habari na
maofisa walioko ngazi za chini kwenye jamii mbalimbali.
Ripoti ya utafiti huo ambayo inaonyesha namna mtu anayehusihwa na imani ya
Ukristo anavyopata matesoyapatikana hapa. Unachoweza kufanya kwa ajili ya
mataifa haya kwa dakika tano tu ni hiki hapa.
Taarifa fupi kutoka utafiti huo.
1. Nigeria;
Taifa hili limegawanyika katika maeneo mawili, kusini na kaskazini, ambapo kusini
mwa nchi hiyo kumekaliwa na wakristo wengi, wakati huko kaskazini kuna idadi kubwa
ya waislamu. Matukio mengi yameripotiwa kutokea eneo la kaskazini ambapo maeneo
yake mengi yanatawaliwa na sheria za kiislamu, ambapo hata hivyo kundi la Boko Haram
limejikita zaidi kuwabadili watu kuwa waislamu, wakishambulia wakristo silaha
mbalimbali ikiwemo mabomu na hata utekaji nyara. Sababu nyingine inaelezwa kuwa
ni uwepo wa kundi la kiislamu la Fulani (Muslim Fulani Herdsmen) ambao huvamia
maeneo ya wakristo na kuwapora ardhi.
2. Syria;
Idadi ya wakristo nchini humu inaripotiwa kuwa chache, na katika kipindi cha kuandaliwa
ripoti ya utafiti huu, ianoyesha kuwa wakristo wengi wameuwawa kutokana na vita
inayoendelea nchini humo, msimamo wa waislamu wenye itikadi kali waliopo
kwenye kamundi yanayoshiriki vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo na pia
hata kuwekwa kati kwa wakristo baina ya makundi ya Shia na Sunni yanayohasimiana.
Aidha wakristo wam
eendelea kuwa kwenye hatihati nchini humo kutokana na kukisiwa kuunga mkono
utawala wa Bashar al-Assad.
3. Misri;
Taifa hili ambalo lipo kwenye mpito, lina idadi kubwa ya wakristo kwa mwamvuli wa
kikoptiki (Coptic Orthodox Christians), linatatizwa na mashambulizi mbalimbali ambayo
yalizidi kushamiri mara baada ya kuondolewa madarakani Rais Mohamed Morsi
mnamo July 2013. Ambapo kikundi cha Muslim Brotherhood pamoja na makundi
mengine yamehusika na mashambulizi hayo ikiwemo kuchoma makanisa na mali
za wakristo nchini humo, na pia mauaji.
4. Jamhuri ya Afrika ya Kati;
Japokuwa taifa hili lina idadi kubwa ya wakristo kulinganisha na makundi mengine,
ripoti inaonyesha kuwa kundi la Séléka limekuwa likilenga jamii ya wakristo,
ikiwemo vijiji, ambapo lengo lao kuu ni kutaka kulibadili taifa hilo kuwa la
kiislamu. Licha ya kwamba mateso yameripotiwa, matukio mengine huenda
kuwa yameachwa kutokana na kutopata usahihi wa taarifa.
5. Mexico;
Ukabila na rushwa imeripotiwa kuwa chanzo kikuu cha mashambulizi kwa wakristo
nchini humu, ambapo licha ya wingi wao, wakristo wamelazimika kuishi kwa
mashaka kutokana na maeneo waliyopo kuongozwa na mila ambazo mtu
akikengeuka huweza kushambuliwa. Na kundi kuu ambalo limekumbwa na
athari hizi ni jamii ya Wapentekoste, Walutheri na pia 'Presbyterian'
No comments:
Post a Comment